Sekretariet ya jumuiya ya waliosoma shule ya sekondari Mzumbe (Mzumbe Secondary School Alumni) inawataarifu wanajumuiya wote kuwa Jumamosi ya Tarehe 29 mwezi Novemba 2014kutafanyika mkutano wa wanachama wote jijini Dar es Salaam, katika ukumbi wa Jolly Club - Isumba Lounge kuanzia saa nane mchana.
Tangu kuanzishwa kwake Jumuiya ya waliosoma Mzumbe Sekondari imeshirikiana na uongozi wa shule hiyo kuainisha maeneo mbalimbali ambayo jumuiya hiyo itashiriki kuyaboresha.
Katika mkutano huo wa wanachama wote, uongozi wa jumuiya utachaguliwa na mpango mkakati wa miaka mitano utajadiliwa.
Mafanikio ya malengo ya kuiboresha Shule ya Sekondari Mzumbe yanaanza na ushiriki wa kila aliyesoma Mzumbe. Upatapo ujumbe huu, tafadhali wafikishie taarifa wanajumuiya wengine.
Kuthibitisha ushiriki wako wa kikao tuma ujumbe kwa etalawa@gmail.com , au SMS to 0784 250 504; 0652 429 308 ; 0767 210 827
Eddy Talawa
Mwenyekiti wa muda,
Jumuiya ya waliosoma shule ya sekondari Mzumbe