Meneja Masoko wa Mfuko                wa GEPF, Bw. Aloyce Ntukamazina akiongea na vyombo vya                habari juu ya mipango ya Mfuko huo kutoa misaada kwa jamii                hasa kwa wale wenye mahitaji kama walemavu wa ngozi                (Albino) 
                Mtoto Maria Mwingira                akipokea msaada wa mafuta maalum ambayo hukinga ngozi yao                wakati wa jua kali kutoka kwa Meneja Masoko wa GEPF, Bw.                Aloyce Ntukamazina.
                Kijana Salum Iddi akitoa                neno la shukurani kwa Mfuko wa GEPF kwa niaba ya watoto                wenzake huku akisikilzwa kwa makini na Meneja Masoko wa                GEPF, Bw. Aloyce Ntukamazina pamoja na Afisa Uendeshaji wa                Mfuko huo,Bi. Zuwena Rajabu.
                Afisa kutoka GEPF,Bw.                Gaudence Mkoba akikabidhi misaada hiyo kwa wanafunzi wa                shule ya msingi ya Matumaini. 
                Mkurugenzi wa Shule ya                Msingi ya Matumaini Bw. Chacha akizungumza na baadhi ya                watoto wa shule hiyo huku mwenyekiti wa umoja wa Albino                wilaya ya Ilala Bw Seif Ulate akifuatilia kwa makini.