Kafulila: Tunajadili kifo cha aliyekuwa waziri wa Fedha na siyo baba wa mbunge humu ndani, yule alikuwa ni kiongozi wetu
Mpina: Makosa makubwa yamefanywa na Mwanasheria mkuu na Katibu mkuu wa wizara ya madini.
Mpina: Fedha zilizoibiwa za Watanzania ni nyingi sana.
Mpina: Ni bahati mbaya tuna Profesa muongo kama Muhongo ambaye ni Waziri wa Nishati na Madini
Filikunjombe: Kwanza mnasema si fedha za umma lakini magari yote ya Tanesco yameandikwa SU, sasa SU sijui maana yake nini?
Filikunjombe: Kama tumefika mahala tunakanusha namna hii basi inabidi wale viongozi wote tuliowawajibisha tuwaombe radhi.
Filikunjombe: Tanesco kwa miaka 11 wamesema kuna fedha yetu humu ndani, sasa leo kikao kimoja tu wanasema hataa hatuna fedha?
Filikunjombe: Swali la 1 kwa CAG pesa ni ya nani, na alijibu kuwa mle ndani kulikuwa na fedha ya kodi hivyo ni pesa ya umma.
Mwanasheria Mkuu: Nawaomba radhi sana Majaji maana hli jambo nilitaka liishe kabla ya christmass.
Mwanasheria Mkuu: Sijitetei ni kweli jambo hilo nililifanya kwa mujibu wa sheria na ninasimamia jambo hilo hadi leo.
Mwanasheria Mkuu: AG hakusamehe kodi ya VAT kama ambavyo ripoti inasema.
Mwanasheria Mkuu: Maelezo ya CAG, TAKUKURU na PAC hakuna maelezo ya moja kwa moja kuwa fedha hizi ni za umma.
Mwanasheria Mkuu: Mimi kwa msimamo wangu ni kwamba fedha hizi sio za umma.
Mwanasheria Mkuu: Kwanza aliondoa lile suala la ufilisi, pili alitengua ufilisi wa muda.
Mwanasheria Mkuu: Kuna mambo matatu makubwa, na labda nianze na chanzo cha haya.
Mwandosya: Fedha hizi zimo katika hesabu ya benki kuu ndio maana Gavana mkuu alikuwa na wasiwasi katika kuzitoa fedha hizi.
Mwandosya: Suala hili linatuondolea sifa kama nchi, linatuondolea heshima kama taifa, kimataifa na mbele za wananchi.
Wasira: TAKUKURU iwachambue watu wote bila kujali vyama au nini ili tuwapeleke kwenye sheria.
Wasira: Nchi ambayo unaenda na sandarusi, mabox kubeba hela, hapa hatuna nchi, inabidi TAKUKURU watutajie ni kina nani hawa.
Wasira: Tutakuwa Bunge la ajabu kama maneno haya yameandikwa na vyombo hivi vya Bunge halafu sisi tukalifumbia macho.
Wasira: Afadhali kuwa maskini mwenye heshima kuliko tajiri anayetukanwa.
Wasira: Sisi bunge hili lazima tunangalie maslahi ya Watanzania, hatuwezi kutumiwa na mtu.
Wasira: Kama kuna mtu anataka kuwa Rais na mbinu zake ni kuondoa wengine huyo hafai kabisa kuwa Rais wa Tanzania
Wasira: Jambo la pili ni wajibu sasa wa Bunge hili kutazama ripoti hizi na kuzifanyia kazi.
Wasira: CAG sio mara ya kwanza kuchunguza na kuleta taarifa bungeni, na PAC nao hii ni kazi yao kuchunguza na kuleta Bungeni
Shibuda: Ripoti ya Waziri Muhongo jana imemnasua Waziri mkuu na sakata hili .