Kama hukusikiliza ama kuangalia kikao cha Bunge leo Novemba 10, moja ya mambo yaliyozungumziwa ni pamoja na suala kukosekana kwa dawa katika Hospitali kutokana na bohari kuu kusitisha huduma ya kusambaza dawa pamoja na matibabu ya Rais Dkt. Kikwete Marekani.
".. Kutokana na Serikali kudaiwa bilioni 102 na bohari ya madawa MSD hali ya Hospitali zetu ni mbaya sana.. wagonjwa wanaendelea kuteseka na maradhi, madawa hamna.. wanawake wanakufa, watoto wanateseka.. huku sisi waheshimiwa wabunge tukiendelea kukaa humu tukila viyoyozi'
'kwa taarifa tulizonazo Mheshimiwa Rais yupo nje kaenda kuchekiwa afya yake.. Ili tuwatendee haki Watanzania waliotuweka katika bunge hili na tuweze kuokoa maisha yao naomba bunge lako liahirishe shughuli zinazoendelea tuweze kujadii jambo hili kwanza.. tulipatie ufumbuzi kwa maslahi ya Watanzania.. na kwa maana hiyo naomba kutoa hoja na waheshimiwa wabunge naomba mniunge mkono.." – Rukia Ramadhani, mbunge viti maalum CUF.
Mbunge Ally Kessy akajibu hoja hiyo;- "..Wabunge wangapi wa upinzani tayari wameshawahi kwenda India mara sita.. Kwa majina nawajua tena wa CUF wamekwenda India kutibiwa mara tatu mara nne leo mnazungumzia habari ya Rais kwenda kutibiwa Marekani, aende kutibiwa wapi Zanzibar? Acheni mambo yenu hayo.."
Naibu Spika wa Bunge akafunga mjadala huo;- "..Waheshimiwa wabunge ningewaomba sana kuhusiana na masuala ya wagonjwa wetu mbalimbali wawe ni wabunge.. Awe ni mheshimiwa Rais na wanatibiwa wapi.. Naliomba jambo hili tuliache litatuharibia hali ya hewa bila sababu jamani.. Nawaombeni sana hilo nimelitoa katika utaratibu na kwenye hansard tulifute jamani.."- Job Ndugai.