Waziri wa Viwanda na Biashara,Mh. Dkt. Abdallah Kigoda akipata maelezo ya namna ya kunufaika baada ya kujiunga na Mfuko wa Mafao ya Kustaafu GEPF kutoka kwa Afisa Masoko wa Mfuko huo, Albert Kitunga, wakati alipotembelea banda la maonesho la GEPF kwenye maonyesho ya siku ya viwanda yanayoendelea kwenye viwanja vya maonyesho ya Kimataifa ya Biashara 'sabasaba' Dar es Salaam.
Afisa Masoko wa Mfuko wa GEPF, Albert Kitunga akimuonyesha Waziri wa Viwanda na Biashara,Mh. Dkt. Abdallah Kigoda fomu za kujiunga na Mfuko huo wakati alipotembelea banda la maonesho la GEPF kwenye maonyesho ya siku ya viwanda yanayoendelea kwenye viwanja vya maonyesho ya Kimataifa ya Biashara 'sabasaba' Dar es Salaam.
Wafanyakazi wa Mfuko wa Mafao ya Kustaafu GEPF wakitoa huduma kwa mmoja wa wateja wao mbalimbali kwenye maonyesho ya siku ya viwanda yanayofanyika kwenye viwanja vya maonesho ya Biashara ya Kimataifa 'sabasaba' Dar es Salaam.