Wiki hii, Ubalozi ukiongozwa na Mama Balozi Rose Mero umeshiriki kwenye maonyesho ya UN ya kina mama, Geneva (United Nations Women's Guild 2014), yenye lengo la kukusanya pesa za kusaidia miradi ya kuendeleza watoto wenye mahitaji mbalimbali duniani kote.
Kwenye maonyesho hayo, banda la Tanzania lilijumuisha bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na kutengenezwa nchini Tanzania ikiwa ni pamoja na kahawa, majani ya chai, khanga, vitenge, vinyago, korosho n.k
Watu mbalimbali walipata nafasi ya kujipatia chakula cha kitanzania kama vile maandazi, chapatti, samaki wa kukaanga, maharage ya kuungwa na Nazi, chai yenye viungo vya tangawizi, sambusa, pilau, n.k