Tuesday, November 25, 2014

BENKI YA WANAWAKE TANZANIA (TWB) YATOA HATI ZA VIWANJA KWA WATEJA WAKE



BENKI YA WANAWAKE TANZANIA (TWB) YATOA HATI ZA VIWANJA KWA WATEJA WAKE
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki  ya Wanawake  Tanzania (TWB), Magareth Chacha  (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichai) wakati wa hafla ya kukabidhi hati za viwanja kwa wateja walionunua na waliomaliza kulipa mikopo yao, Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja Masoko wa Benki hiyo, Aaron Nyanda na Mwanasheria wa Ardhi Plan Ltd, Musa Maghimbi. (Picha na Francis Dande) 
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki  ya Wanawake  Tanzania (TWB), Magareth Chacha  (wa pili kushoto) akimkabidhi hati ya kiwanja, Mhindi Mayenga wakati wa hafla ya kukabidhi hati za viwanja kwa wateja walionunua na waliomaliza kulipa mikopo yao, Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja Masoko wa Benki hiyo, Aaron Nyanda na kulia ni Mwanasheria wa Ardhi Plan Ltd, Musa Maghimbi. 
Wateja wa Benki ya Wanawake Tanzania (TWB) wakiwa wameshika hati zao za viwanja baada ya kukabidhiwa na uongozi wa benki hiyo. Kutoka kushoto ni Belinda Rweyemamu, Mhindi Mayenga na Gabriel Kameka.