Friday, November 21, 2014

ASHAURI KUBADILI MFUMO WA ULIPAJI FIDIA YA ARDHI



ASHAURI KUBADILI MFUMO WA ULIPAJI FIDIA YA ARDHI
Serikali imetakiwa kubadilisha mfumo wa zamani wa ulipaji fidia kwa wananchi na kutumia mfumo wa kisasa, ili mwananchi aweze kufaidika na ardhi yake baada ya kupimwa.

Mkurugenzi wa Kampuni ya World Map Consultants Limited inayojishughulisha na upimaji wa ardhi katika mji mdogo wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe, Steven Kyaruzi alisema hayo baada ya kuwakabidhi mikataba ya upimaji wananchi wa eneo maalumu la Viwanda Visegese.
Kyaruzi alisema mfumo na sera ya ushirikiano na ushirikishwaji katika kutoa huduma kwa wananchi kati ya Serikali, sekta binafsi na Wananchi (Public, Private Partnership Model) utasaidia kuinua maisha ya wananchi nchini.
Alisema kampuni yake imepewa jukumu na Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe la uendelezaji wa Mji Mdogo wa Kisarawe kwa kazi ya kuwapimia viwanja wananchi kwa kutumia mtindo wa kisasa katika ulipaji wa fidia, ambapo kila mwananchi ataweza kufaidika na ardhi yake kwa faida na kumwinua katika kipato kwa kutumia ardhi iliyopimwa.
Mkurugenzi huyo alisema mikataba ijayo ni ile ya maeneo ya makazi kwa hiyo kampuni iko kwenye hatua za mwisho za umaliziaji ikiwa tayari kila mwananchi atapata mkataba wake ili aweze kumiliki ardhi yake iliyopimwa.
Naye Mosesi Mwasha wa Kijiji cha Visegese alisema kampuni hiyo ni mkombozi kwao kwani walikuwa hawajui kama ardhi ikipimwa inakuwa na thamani kubwa. hivyo kwa mfumo huo ataweza kuongeza kipato chake na familia