Sunday, November 30, 2014

Wakazi wakaskazini wanufaika na Gulio la Vodacom Tanzania


Wakazi wakaskazini wanufaika na Gulio la Vodacom Tanzania
 Afisa Mauzo wa Duka la Simu la Bei nzuri la jijini Arusha,Martha  Meena akitoa maelezo kwa wateja waliofika katika banda la duka hilo  wakati wa gulio la punguzo kubwa la bei za bidhaa za Mawasiliano   lijulikanalo kama Vodacom Expo linalofanyika siku mbili katika uwanja wa Sheakh  Amri Abeid jijini Arusha.
 Afisa huduma kwa wateja wa Duka la  Vodacom jijini Arusha,Samya Ulimwengu  akitoa maelezo kwa mmoja wa wateja waliofika katika banda lao   kujipatia huduma za mawasiliano ambazo zinapatikana katika Gulio la Vodacom Expo kwa punguzo kubwa la bei lililofanyika katika uwanja wa Sheakh Ami Abeid jijini Arusha. 


Mamia ya wakazi wa jiji la Arusha wakiwa katika Gulio la Vodacom Expo kupata   huduma mbalimbali za mawasiliano ambazo zimeuzwa kwa punguzo kubwa la bei lililofanyika kwa siku mbili katika  uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.


RAIS DKT SHEIN AZUNGUMZA NA VIONGOZI WA CHAMA CHA CCM KASKAZINI UGUJA



RAIS DKT SHEIN AZUNGUMZA NA VIONGOZI WA CHAMA CHA CCM KASKAZINI UGUJA
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Viongozi katika Mkoa wa Kaskazini Unguja akiwa katika jitihada zake za kuimarisha Chama cha Mapinduzi (CCM) katika Mkoa huo,(kulia) Naibu Katibu Mkuu CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai, na  wa kwanza (kushoto) Mjumbe wa Kamati Kuu CCM Taifa Khadija Hassan Aboud akifuatiwa na Mwenyekiti wa CCM Kaskazini A Unguja  Ali Makame Khamis, sambamba na jitihada hizo leo anatarajiwa kuanza kuzungumza na Viongozi mbali mbali wakiwemo Mabalozi na Wenyeviti wa Maskani wa Chama hicho katika Mikoa  ya Pemba.  [Picha na Ikulu.]



TANZANIA 50 PLUS CAMPAIGN WATEMBELEA WAGOJWA WA SARATANI WALIOLAZWA HOSPITAL YA OCEAN ROAD



TANZANIA 50 PLUS CAMPAIGN WATEMBELEA WAGOJWA WA SARATANI WALIOLAZWA HOSPITAL YA OCEAN ROAD
Mgeni rasma ambaye ni DR kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Amana DR. Natalius Kapilima akikata utepe kuashilia kugawa zawadi mbalimbali kwa wagojwa wa saratani waliolazwa katika hospital ya ocean road wengine kushoto ni Mkurugenzi wa TTCF. Lutgard Kagaruki na wa tatu kulia ni Mratibu wa kampeni ya manusura wa saratani ya Tezi Dume na Mwanzilishi wa Tanzania 50 Plus Campagn Dr Emanuel Kandusi
DR kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Amana DR. Natalius Kapilima kulia akimkabizi zawadi mgojwa wa saratani Idd Muhode ambaye amelazwa katika hospitali ya ocean road
Baadhi ya wadau mbalimbali wa kujitolea kutoka Tanzania 50 plus campaign wakiwa katika picvha ya pamoja baada ya kutoa misaada mbalimbali kwa wagojwa wa saratani katika hospital ya Ocean Road.

DR kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Amana DR. Natalius Kapilima akipokea zawadi za wagojwa zilizoenda kugawiwa katika hospitali ta Ocean Road kutoka kwa
Mratibu wa kampeni ya manusura wa saratani ya Tezi Dume na Mwanzilishi wa Tanzania 50 Plus Campagn Dr Emanuel Kandusi mwingine ni
Mkurugenzi wa TTCF. Lutgard Kagaruki walipokwenda kutoa misaada mbalimbali kwa wagojwa
vitu mbalimbalio vikipakiwa kwenye mfuko kwa ajili ya kugawa kwa wagojwa
vifurushi vikiwa tayali kwa kugawiwa kwa wagojwa wa saratani katika hospitali ya ocean road
Mratibu wa kampeni ya manusura wa saratani ya Tezi Dume na Mwanzilishi wa Tanzania 50 Plus Campagn Dr Emanuel Kandusi kulia akimkabizi zawadi mgojwa Said Kassam aliyelazwa katika hospital ya Ocean Road


TICTS YAKABIDHI MSAADA WA VITABU KWA SHULE YA MSINGI MIVINJENI JIJINI DAR



TICTS YAKABIDHI MSAADA WA VITABU KWA SHULE YA MSINGI MIVINJENI JIJINI DAR
Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Kampuini ya Ushushaji Mizigo Bandarini Tanzania International Cpontainer Termi nal (Ticts) Paul Wallace akipeana mikono na wanafunzi wa Shule ya Msingi Mivinjeni baaada ya kuwakabidhi msaada wa vitabu.
Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Kampuini ya Ushushaji Mizigo Bandarini Tanzania International Container Terminal (Ticts) Paul Wallace akiwakabidhi Vitabu wanafunzi wa Shule ya msingi Mivinjeni .
Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Ushushaji Mizigo Bandarini Tanzania International Container Terminal (Ticts), Paul Wallace (kushoto) akimkabidhi Moja ya Vitabu walivyokabidhi kwa Mwalimu Mkuu ya Shule ya Msingi Mivinjeni Dar es Salaam, Sabas Selestian juzi wapili (kulia) ni Diwani wa Kurasini, Wilfred Kimath na Mwenyekiti wa Bodi shule hiyo, Elijius Anold.


Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi awahimiza Watanzania kuitumia fursa inayotolewa na Chuo Kikuu Huria cha Tanzania


Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi awahimiza Watanzania kuitumia fursa inayotolewa na Chuo Kikuu Huria cha Tanzania
 Mkamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akitia saini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili Makao Makuu ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania yaliyopo Bungo Kibaha Mkoa wa Pwani kwa ajili ya mahafali ya 26  ya chuo hicho.Aliyesimama ni Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania ambae pia ni Waziri wa Katiba na Sheria Tanzania Dr. Asha – Rose Migiro.
 Balozi Seif akisalimiana na baadhi ya wahitimu wa shahada, stashahada na vyeti wa chuo Kikuu huria cha Tanzania ambao wametokea  Zanzibar .
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif wa pili kutoka kulia waliokaa akiwa katika picha ya pamoja na Wahitimu wa Chuo Kikuu huria cha Tanzania waliosimama nyuma pamoja na Uongozi wa Chuo hicho.Waliosimama wa Pili kutoka kulia ni Mbunge wa Jimbo la Dole Mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar Muhitimu Mh. Selvester Mabunda. Kushoto ya Balozi Seif ni Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Profesa Samuel Wangwe, kulia ya Balozi ni Mkuu wa Chuo ambae pia ni Waziri wa Katiba na Sheria Dr. Asha-Rose Migiro na Makamu Mkuu wa bChuo hicho Profesa Tolly Mbwette.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar akiwa na Mwenyeji wake Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Dr. Asha-Rose Migiro wakiliongoza Gwaride kuingia kwenye uwanja wa Mahafali ya 26 ya chuo kikuu huria cha Tanzania yaliyofanyika Makao Makuu yake Bungo Kibaha, Mkoa wa Pwani. Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.


yale yaleeeee....Gatepass ya Mlimani City, dar es salaam


Hii ni hatari kupita maelezo, sasa KIA na Mlimani City kuna uhusiano gani?????????
yale yaleeeee....Gatepass ya Mlimani City, dar es salaam



KINANA APOKELEWA KWA SHANGWE MTWARA MJINI



KINANA APOKELEWA KWA SHANGWE MTWARA MJINI
 Vijana wa Bodaboda wakiongoza msafara wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakati akiwasili Mtwara mjini ambapo alishiriki shughuli mbali mbali za kujenga na kuimarisha chama pamoja na kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM 2010.
 Msafara wa Katibu Mkuu ukielekea Mtwara mjini.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Mikindani mara baada ya kukabidhi leseni kwa madereva 70 wa boda boda waliohitimu mafunzo chini ya udhamini wa Mbunge wa Mtwara mjini Hasnain Murji
 Wananchi wa Mikindani mkoani Mtwara wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana .
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikabidhi pikipiki kwa vikundi vya Bodaboda zilizotolewa na Mbunge wa Mtwara mjini Hasnain Murji
 Mbunge wa Mtwara mjini Hasnain Murji akihutubia wakazi wa Mikindani baada ya kuwakabidhi leseni madereva 70 wa boda boda na kuwakabidhi pikipiki tatu kama mtaji wa kuendeleza vikundi vyao.
kwa picha zaidi bofya soma zaidi

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ukarabati wa ofisi ya CCM kata ya Majengo iliyochomwa moto wakati wa vurugu za gesi.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ukarabati wa ofisi ya CCM kata ya Majengo iliyochomwa moto wakati wa vurugu za gesi
 Katibu Mkuu wa CCM akiwasalimia wakazi wa kata ya Majengo alipotembelea kujionea maendeleo ya ukarabati wa ofisi ya CCM .
 Wananchi wakishangilia msafara wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana aliyewasili mkoani Mtwara ambaye anategemewa kufanya mkutano mkubwa wa hadhara siku ya Jumapili tarehe 30 Novemba 2014.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimtwisha maji mama mmoja mkazi wa mtaa wa Mwera kata ya Chikongola baada ya kuzindua mradi wa kisima cha maji kilichofadhiliwa na Mbunge wa Mtwara mjini Hasnain Murji
 Katibu Mkuu wa CCM akiangalia kazi za kikundi cha wakina Mama wa Matopeni ambao wapo zaidi ya 200 na wanajishughulisha na shughuli mbali mbali za ujasiriamali Mtwara mjini.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiweka jiwe la msingi la mradi wa ufugaji kuku wa mayai wa kikundi cha akina mama cha Rahaleo.
 Katibu Mkuu wa CCM akiangalia kuku wa mayai wanaofugwa na kikundi cha akina mama wa Rahaleo.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kushona viatu pamoja na fundi viatu Abeid Yusufu Likanga (ambaye ni mlemavu wa miguu) wa kata ya Rahaleo mkoani Mtwara.
 Katibu Mkuu wa CCM ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na viongozi wa chama wakiangalia maendeleo ya uchimbwaji wa mfereji unaopeleka maji baharini katika kata ya Shangani.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikara utepe kuashiria uzinduzi wa tawi la CCM Chuo cha Utumishi wa Umma kwenye ofisi za CCM wilaya ya Mtwara mjini.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akigutubia wanafunzi wa Chuo Cha Utumishi Mtwara mara baada ya kuzindua tawi lao la CCM.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikabidhi Katiba ya CCM kwa Katibu wa Tawi la Chuo Cha Utumishi Mwamvua Patrick.
 Katibu Mkuu wa CCM ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wajumbe wa wa halmashauri kuu ya wilaya ya Mtwara mjini kwenye kikao kilichofanyika ukumbi wa VETA
Katibu Mkuu wa CCM ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wajumbe wa wa halmashauri kuu ya wilaya ya Mtwara mjini kwenye kikao kilichofanyika ukumbi wa VETA ambapo alisisitiza wajumbe wasahau yaliyopita na kusimama kukijenga chama


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu, William Lukuvi wakiteta na Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, Bungeni mjini Dodoma



Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu, William Lukuvi wakiteta na Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, Bungeni mjini Dodoma
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu, William Lukuvi (kushoto) wakiteta na Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, Bungeni mjini Dodoma Novemba 29, 2014.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu, William Lukuvi (kushoto) wakiteta na Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, Bungeni mjini Dodoma Novemba 29, 2014.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu


TANZANIA 50 PLUS CAMPAIGN WATEMBELEA WAGOJWA WA SARATANI WALIOLAZWA HOSPITAL YA OCEAN ROAD



TANZANIA 50 PLUS CAMPAIGN WATEMBELEA WAGOJWA WA SARATANI WALIOLAZWA HOSPITAL YA OCEAN ROAD
Mgeni rasma ambaye ni DR kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Amana DR. Natalius Kapilima akikata utepe kuashilia kugawa zawadi mbalimbali kwa wagojwa wa saratani waliolazwa katika hospital ya ocean road wengine kushoto ni Mkurugenzi wa TTCF. Lutgard Kagaruki na wa tatu kulia ni Mratibu wa kampeni ya manusura wa saratani ya Tezi Dume na Mwanzilishi wa Tanzania 50 Plus Campagn Dr Emanuel Kandusi
DR kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Amana DR. Natalius Kapilima kulia akimkabizi zawadi mgojwa wa saratani Idd Muhode ambaye amelazwa katika hospitali ya ocean road
 








MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AIWAKILISHA TANZANIA KATIKA MKUTANO WA 3 WA WAKUU WA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI (EAC) KUHUSU MIUNDOMBINU JIJINI NAIROBI, KENYA



MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AIWAKILISHA TANZANIA KATIKA MKUTANO WA 3 WA WAKUU WA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI (EAC) KUHUSU MIUNDOMBINU JIJINI NAIROBI, KENYA
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wa tatu kutoka (kushoto) Makamu wa Rais wa Kenya, William Ruto, (kushoto kwake) Makamu wa Rais kwanza wa Burundi, (kulia kwake) wakijumuika kwa pamoja na viongozi  wengine wakionyesha Taarifa ya pamoja waliyoisaini kuhusu majadiliano ya kuimarisha Miundombinu kwa nchi wanachama wa  Jumuiya ya Afrika Mashariki, katika mkutano wa 3 wa Wakuu wa Nchi za Afrika Mashariki (EAC) kuhusu Miundombinu, uliofanyika kwenye Ukumbi wa KICC, jijini Nairobi jana Novemba 29, 2014. Picha na OMR.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza katika mkutano wa 3 tatu wa wakuu wa Nchi za Afrika Mashariki (EAC) kuhusu miundombinu, uliofanyika katika ukumbi wa KICC jijini Nairobi jana Novemba 29, 2014. Picha na OMR.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na baadhi ya viongozi wakati  wakitoka kwenye Ukumbi wa mikutano wa KICC, baada ya kushiriki katika mkutano wa 3 wa Wakuu wa Nchi za Afrika Mashariki (EAC) kuhusu Miundombinu uliofanyika jijini Nairobu, Kenya jana Novemba 29, 2014.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na viongozi 
wengine walioshiriki katika mkutano huo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, kifurahia jambo na Makamu wa Rais wa  Kenya William Ruto na Waziri wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, wakati wakiondoka katika viwanja vya Ukumbi wa mikutano wa KICC, baada ya kushiriki kwenye mkutano wa 3 wa Wakuu wa Nchi za Afrika Mashariki (EAC) kuhusu Miundombinu, uliofanyika jijini Nairobi, Kenya jana Novemba 29, 2014. Picha na OMR

MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA AIWAKILISHA TANZANIA KATIKA MKUTANO WA WAKUU WA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI (EAC) KUHUSU MIUNDOMBINU JIJINI NAIROBI, KENYA
Mheshimiwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal jana Novemba 29, 2014 aliiwakilisha Tanzania katika mkutano wa siku moja wa Wakuu wa Nchi zinazounda Jumuiya ya Afrika Mashariki jijini Nairobi, Kenya. Mkutano huo, kwa mujibu wa utaratibu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, unafanyika kila baada ya miaka miwili na lengo lake kuu ni kufanya tathmini juu ya miradi ya miundombinu inayoshirikisha nchi washirika, sambamba na kutazama fursa ya kutanua miundombinu mipya katika nchi hizi kwa lengo la kukuza uchumi wa pamoja kwa nchi za Afrika Mashariki.
Tathmini hii ya Miundombinu inafanyika kwa kuwa mataifa ya Afrika Mashariki yanatambua umuhimu wa kuwa na miundombinu bora katika nchi hizi ili kuharakisha ukuaji wa uchumi, sambamba na kutanua mtengamano wa nchi hizi na hivyo kuwafanya wananchi wanaoishi ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kuzidi kuwa wamoja.
Mkutano wa jana uliongozwa na Kaimu Rais wa Kenya Mheshimiwa William Ruto na kuhudhuriwa na Mheshimiwa Makamu wa Rais Dkt. Bilal, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Burundi, Waziri Mkuu wa Rwanda pamoja na Waziri wa Afrika Mashariki wa Uganda. Viongozi wengine waliopata nafasi ya kuhudhuria mkutano huo ni pamoja na Mheshimiwa Balozi Richard Sezibera, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na Waziri wa Wizara hiyo kutoka Tanzania, Mheshimkiwa Samwel Sitta, Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika, Dkt. Donald Kaberuka, Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Ukanda wa Afrika, Bwana Makhtar Diop, Katibu Mtendaji wa UNCTAD, Dkt. Mukhisa Kituyi na Baalozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania Balozi Filiberto Sebregondi. Pia mkutano huo ulihudhuriwa na wawakilishi wa nchi za China, Marekani, Japan na nyinginezo ambazo ni wadau wakubwa wa ujenzi wa miundombinu katika nchi za Afrika Mashariki.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo, Kaimu Rais wa Kenya, William Ruto alifafanua juu ya umuhimu wa kuhakikisha Afrika Mashariki inaunganishwa kwa miundombinu imara ili kukuza uchumi na akapongeza jitihada mbalimbali zinazofanyika katika kufanikisha azma hiyo huku pia akiomba nchi wanachama wa Afrika Mashariki kuendelea kuungana katika kutekeleza miradi ya miundombinu na kujitahidi kutafuta fedha kwa ajili ya kukamilisha miradi hiyo.
Mkutano huu pia uliambatana na kupokea ripoti ya utekelezaji wa maagizo ya Wakuu wa Nchi za EAC kuhusu Miundombinu kutoka kwa Mawaziri wa Nchi za Jumuiya.  Wakuu wa Nchi katika Mkutano huu walipokea taarifa ya utekelezaji wa maagizo waliyoyatoa katika mkutano wa pili uliofanyika mwezi Novemba, 2012 na kuidhinisha miradi 72 ya miundombinu ya kipaumbele ya Barabara, Reli, Nishati na Bandari.
Kwa upande wa utekelezaji; miradi 16 imekamilika, 39 inaendelea kutekelezwa na 17 ipo katika hatua za awali za kutafutiwa fedha kwa ajili ya utekelezaji wake.
Kwa upande wa Tanzania miradi minne imekamilika ambayo ni Umeme katika mji wa Kibondo, mradi wa barabara ya Mbezi-Shule-Tangibovu-Makutano ya Nelson Mandela na barabara ya Tabata. Barabara nyingine iliyokamilika ni Nyangunge – Musoma – Sirari na sehemu ya Simiyu - Musoma inayounganisha Kenya na Tanzania huko ujenzi unaendelea.
Akizungumza katika Mkutano huo Makamu wa Rais amezitaka nchi wanachama kuharakisha utekelezaji wa miradi ya Miundombinu ili kusaidia utekelezaji wa Itifaki ya Soko la Pamoja, ambayo inalenga kurahisisha usafirishaji wa bidhaa na abiria. "Tusiishie kubakiza mipango hii katika karatasi, tusiishie kuzungumza tu bali huu ni wakati wa kuhakikisha tunarahisisha ufanyaji biashara katika nchi zetu na kupunguza vikwazo visivyo vya lazima," alisema Mheshimiwa Makamu wa Rais.
Katika mkutano huo, Mheshimiwa Makamu wa Rais pia aliambatana na Mheshimiwa Dkt. Mahadhi J. Maalim, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa pamoja na Waziri wa Viwanda na Biashara wa Zanzibar, Mheshimiwa Nassor Ahmed Mazrui. Mheshimiwa Makamu wa Rais na msafara wake tayari wamerejea nyumbani Tanzania ambapo kesho anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani, maadhimisho yanayofanyika Kitaifa Mkoani Njombe.
Imetolewa na: Ofisi ya Makamu wa Rais
Novemba 30, 2014