Tuesday, October 21, 2014

WAKULIMA WA ZAO LA SHAYIRI WATEMBELEA KIWANDA CHA KIMEA CHA TBLMOSHI


WAKULIMA WA ZAO LA SHAYIRI WATEMBELEA KIWANDA CHA KIMEA CHA TBLMOSHI
 MENEJA wa Kiwanda cha Kimea - Moshi, Vitus Mhus akiwaonyesha hatua ya kwanza ya zao la Shayiri linalotumika kutengenezea kimea mahali linapopokelewa kabla ya kuanza kuingizwa kiwandani.Wakulima hao kutoka Vyama Nane vya Ushirika vya wilaya ya Karatu na Monduli mkoani Arusha walitembelea kiwandani hapo hapo juzi ili kujifunza na kujionea zao wanalolima linaandaliwa vipi hadi kutengeneza Kimea
 wakulima wa zao la Shayiri kutoka Vyama Nane vya Ushirka vya wilaya ya Karatu na Monduli mkoani Arusha wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kusikiliza maelezo namna ya kulima Shayiri yenye ubora kutoka kwa Meneja  Mradi Kilimo cha Shayiri Dk. Basson Bennie. Wakulima hao walifurahia ziara iliyofanywa kwenye Kiwanda cha kuzalisha Kimea kilichopo mjini Moshi ambapo waliahidi kulima Shayiri yenye ubora zaidi katika msimu ujao.
 Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Bia nchini (TBL), Edith Mushi akiwapa maendelekezo wakulima wa zao la Shayiri waliotembelea Kiwanda cha kuzalisha Kimea mjini Moshi namna ya kutembelea ndani ya kiwanda ili wajionee namna Shayiri inavyozalishwa na kuwa Kimea.Wakulima hao wanatoka kwenye vyama Nane vya Ushirika vilivypo wilaya ya Karatu na Monduli mkjoani Arusha
 Meneja wa Kiwanda cha Kimea-  Moshi Vitus Mhusi akiwaonyesha wakulima wa Shayiri waliofanya ziara ya kutembelea kiwanda hicho namna uchafu unavyochambuliwa kutoka kwenye Shayiri wanayolima mashambani, ambapo aliwaomba kujitahidi kuhakikisha inakuwa safi wakati wa mavuno.
  Pichani ni Meneja wa Kiwanda cha Kimea kilichopo mjini Moshi akiwaonesha wakulika kutoka Vyama vya Ushirika Nane vya Wilaya ya Karatu na Monduli wanaolima Shayiri namna ambavyo uzalishaji wa kimea unavyofanyika, wakati wa ziara yao.
Meneja wa Kiwanda cha Kimea kilichopo Moshi, Vitus Mhusi akiwaonyesha wakulima wa Shayiri namna Kimea kinavyozalishwa wakati wa ziara yao kiwandani hapo. Vingozi hao wa Vyama vya Ushirika Nane kutoka wiayani Monduli na Karatu mkoani Arusha walitembelea kiwandani hapo kwa leng la kujifunza zaidi namna ya kulima zao la Shayiri lenye ubora zaidi na hata kufikia mahitaji ya kiwanda ya Tani 12,000