Saturday, October 11, 2014

Ubalozi Wa Tanzania Japan Waipaisha Kahawa Kilimanjaro Kwenye Treini Ziendazo Kasi Japan


Ubalozi Wa Tanzania Japan Waipaisha Kahawa Kilimanjaro Kwenye Treini Ziendazo Kasi Japan
Kahawa ya Tanzania imekuwa kivutio kikubwa kufuatia ushirikiano wa Ubalozi wa Tanzania Japan na Kampuni binafsi ya M.M. (wauzaji wakubwa wa kahawa ya Kilimanjaro Japan) kuandaa "Special Premium kilimanjaro Coffee Brand " na kuingia makubaliano na Shirika kongwe la treini ziendazo kasi (Bullet Train) la Tokaido JR Shinkansen. Kahawa hiyo imekuwa kiburudisho kikubwa kwa wasafiri wote wanaotumia usafiri huo ambao ni maarufu sana Japan katika miji mbalimbali. Kwa watumiaji wa usafiri huo wanapoingia katika treini hizo unakaribishwa na matangazo maalum kuhusu kahawa hiyo.

Tanagazo la kahawa hii linasomeka kama ifuatavyo :

" In commemoration of the 50th Anniversary of the JR (Japan Railway) Tokaido Shinkansen, we deliver this grade AA Kilimanjaro Coffee from Tanzania which also celebrates its 50th anivessary of the country founding. Please enjoy the fresh acidity and flavor this cup featuring designs from Tingatinga Art of Tanzania"

Kahawa hii maalumu imetengenezwa mahususi kwa ajili ya kusherehekea miaka 50 tangu kuzinduliwa wa treini ya kwanza iendayo kasi Japan sambamba na Tanzania kusherehekea miaka 50 ya Muungano.

Imetolewa na Ubalozi wa Tanzania Japan
Octoba, 2014