Thursday, October 02, 2014

MTENDAJI MKUU PDB AWAPA CHANGAMOTO WAKUU WA MIKOA NA WILAYA



MTENDAJI MKUU PDB AWAPA CHANGAMOTO WAKUU WA MIKOA NA WILAYA
Mtendaji Mkuu kutoka Ofisi ya Rais-Ufuatiliaji wa Utekelezaji wa Miradi (PDB) inayoratibu Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN), Bw. Omari Issa akiwapa changamoto leo Alhamisi Wakuu wa Mikoa na Wilaya (hawapo pichani) kufanya uamuzi wa haraka katika utekelezaji wa majukumu yao na kutosubiri mpaka wafuatiliwe.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Fatuma Mwasa na viongozi wengine wakifuatilia hotuba ya Mtendaji Mkuu wa PDB, Bw. Omari Issa mjini Dodoma leo Alhamisi aliyekuwa akiwakumbusha watendaji hao waandamizi umuhimu wa kuchukua uamuzi kwa haraka na kutosubiri kufuatiliwa katika mambo ambayo yamo ndani ya uwezo wao.
Baadhi ya Wakuu wa Mikoa, Wilaya na watendaji waandamizi waliohudhuria Semina iliyoandaliwa na Ofisi ya Waziri Mkuu wakimsikiliza Mtendaji Mkuu wa PDB, Bw. Omari Issa (hayupo pichani) alipokuwa akitoa mada kuhusu uwajibikaji mjini Dodoma leo Alhamisi.
Mtendaji Mkuu wa PDB, Bw. Omari Issa akijadiliana jambo na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecki Sadiq walipokutana leo Alhamisi mjini Dodoma wakati wa semina inayoendelea kwa Wakuu wa Mikoa, Wilaya na maofisa waandamizi. (Picha zote kwa Hisani ya Ofisi ya Rais-PDB).