Thursday, October 02, 2014

KATIBU MKUU WIZARA YA MAMBO YA NDANI AZINDUA BARAZA DOGO LA WAFANYAKAZI JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI MJINI BAGAMOYO LEO



KATIBU MKUU WIZARA YA MAMBO YA NDANI AZINDUA BARAZA DOGO LA WAFANYAKAZI JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI MJINI BAGAMOYO LEO
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (kushoto) akizungumza na wajumbe wa Baraza Dogo la Wafanyakazi la Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kabla ya kulizindua Baraza hilo katika Hoteli ya Livingstone mjini Bagamoyo leo. Katika hotuba yake, Abdulwakil aliwataka viongozi wakuu wa jeshi hilo kushirikiana kikamilifu na watumishi wote ili kuleta mabadiliko chanya ndani ya jeshi hilo. Wapili kulia ni Kamishna Jenerali wa Jeshi hilo, Pius Nyambacha, Kulia ni Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) tawi la Zimamoto na Uokoaji, Shwaybu Mohamoud. Watatu kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Tume ya Usuluhishi na Upatanishi (CMA), Andrew Mwalisisi na wapili kushoto ni Katibu wa Tughe tawi hilo, Andason Kalewa.
Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Kamishna Jenerali, Pius Nyambacha (kushoto) akitoa hotuba fupi ya kumkaribisha mgeni rasmi Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (wapili kulia-meza kuu) kuzungumza na kulizindua Baraza Dogo la Wafanyakazi la Jeshi hilo. Kulia ni Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (Tughe) tawi la Zimamoto na Uokoaji, Shwaybu Mohamoud. Watatu kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Tume ya Usuluhishi na Upatanishi (CMA), Andrew Mwalisisi na wapili kushoto ni Katibu wa Tughe tawi hilo, Andason Kalewa. Uzinduzi wa Baraza hilo ulifanyika katika Hoteli ya Livingstone mjini Bagamoyo leo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (watano kushoto- waliokaa), Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara hiyo, Lilian Mapfa (watano kulia), Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Kamishna Jenerali, Pius Nyambacha (wanne kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Baraza Dogo la Wafanyakazi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji baada ya kuzinduliwa baraza hilo katika Hoteli ya Livingstone mjini Bagamoyo leo. Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.