Friday, October 03, 2014

MAELFU YA WAKAZI WA TUNDURU WAJITOKEZA KUMPOKEA PROF IBRAHIM LIPUMBA



MAELFU YA WAKAZI WA TUNDURU WAJITOKEZA KUMPOKEA PROF IBRAHIM LIPUMBA
 
Dereva Boda boda ambao ni wananchama wa Chama cha Wananchi CUF wakiongoza msafara wa mapokezi ya Prof Ibrahim Lipumba mara tu alipo wasili Wilayani Tunduru akitokea Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma.Lipumba yupo Mikoa ya Kusini inayojumuisha Ruvuma,Lindi na Mtwara  kwa  ziara ya siku 16 ikiwa na dhumuni la kuimarisha chama pamoja kuhamasisha wananchi  kujitokeza  katika daftari  la  wapiga  kura na vitambulisho  vya  taifa
 Huu ni umati wa watu waliojipanga barabarani kumpokea prof Ibrahim Lipumba
 Wakazi wa Tunduru ambao ni wanachama wa Chama cha Wananchi CUF, wakiwa katika msafara wa Mwenyekiti wa chama  hicho,Prof Ibrahim Lipumba
 
Wanachama wa Chama cha Wananchi CUF wakiwa katika msafara wa mapokezi ya Mwenyekiti wa chama hicho,Prof Ibrahim Lipumba


Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF,Prof Ibrahim Lipumba mwenye shati jekundu na kofia nyekundu akiwapungia mkono wanachama wa chama cha CUF mara tu baada ya kufika katika ofisi za CUF Wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma
 Polisi wakiwa katika ulinzi wa Prof Ibrahim Lipumba


Naibu Mkurugenzi wa Oganaizesheni Uchaguzi na Bunge wa Chama Cha Wananchi CUF – Shaweji Mketo akiwahutubia  wakazi wa wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma,kutokufanya makosa  wakati  wauchaguzi wa serikali  za mitaa uliotangazwa  kufanyika Disemba 14 mwaka huu wahakikishe wanakipigia Chama cha Wananchi CUF
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF,Prof Ibrahim Lipumba akiwahutubia maelfu ya wananchi waTunduru waliojitokeza kumsikiliza katika mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja baraza  la Iddi Tunduru mjini.