Thursday, October 30, 2014

Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji yatembelea Bwawa la Kuzalisha Umeme la Merowe,nchini Sudan



Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji yatembelea Bwawa la Kuzalisha Umeme la Merowe,nchini Sudan
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji imetembelea Bwawa la Kuzalisha Umeme la Merowe katika Mji wa Merowe na kujionea namna ya wenyeji wanavyotumia maji ya Mto Nile kwa kuzalisha umeme wa kutosha kwa ajili ya mji huo na nchi nzima ya Sudan.

Mradi wa Bwawa la Merowe ni mkubwa katika nchi ya Sudan na mbali na kuzalisha umeme, pia unatumika kwa shughuli za kilimo cha umwagiliaji ambacho kwa aslimia mia kinategemea Mto Nile.

Aidha, mradi wa bwawa hilo pia umechangia kuleta maendeleo makubwa kiuchumi kwa kuwezesha kujengwa kwa uwanja bora wa ndege wa kisasa, hospitali bora ya kisasa na kiwanda kikubwa cha nyama ya kuku katika mji wa Merowe.

Hivyo, kuonyesha jinsi gani nchi ya Sudan inavyotumia fursa ya maji ya Mto Nile vizuri katika kuleta maendeleo ya Sekta zote nchini mwao.

Hii ni muendelezo wa ziara ya siku nne nchini humo kwa kamati hiyo, katika kujifunza namna ya kutumia vizuri rasilimali ya maji ya Mto Nile katika kukuza maendeleo ya nchi.
Waziri wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji, Prof. Peter Msolla wakiwa kwenye kiwanda cha nyama ya kuku wakiangalia utendaji na uendeshaji wake.
Mjumbe wa Kamati, Prof. David Mwakyusa akiangalia moja ya kifaa cha kisasa katika Hospitali ya Mji wa Merowe.
Ujumbe wa Tanzania ukisikiliza taarifa ya Mji wa Merowe kutoka kwa Inj. Mohamed Elsheikh.
Mtambo wa kuzalisha umeme katika Bwawa la Merowe.
Ujumbe wa Tanzania, viongozi wa Sudan na wataalam mbalimbali wa Bwawa la kuzalisha umeme la Merowe wakiwa katika picha ya pamoja katika bwawa hilo.
Ndani ya jengo la bwawa la kuzalisha umeme la Merowe.