Muuguzi aliyewekwa chini ya karantini alipowasili Marekani baada ya kuwatibu wagonjwa wa Ebola nchini Sierra Leone ametishia kutoka nyumbani kwake alikozuiliwa iwapo masharti ya kumzuilia hayataondolewa.
Kaci Hickox, ambaye hadi kufikia sasa amekuwa akishirikiana na maafisa wa afya wa jimbo la Maine, anasema kuwa yeye ni mzima kabisa na hana dalili zo zote za maradhi hayo.
Hali yake imemulika tofauti kubwa zilizopo kati ya idara za afya za Serikali ya Taifa na Serikali za majimbo katika kukabiliana na Ebola.
Wanasayansi wanaoshauri Serikali kuu juu ya Ebola wanasema kuwa hakuna haya ya kutumia karantini kama hatua ya kuzuia ugonjwa huo kusambaa.
Hata hivyo maafisa wa afya wa jimbo lake la Maine wametishia kwenda mahakamani kupata idhini ya kuwatumia wanajeshi kuhakikisha haondoki nyumbani kwake iwapo atatisha kufanya hivyo.
VIA-BBC