Tuesday, October 14, 2014

CRDB Lumumba, Yaadhimisha Siku ya Huduma kwa Wateja Kwa Kuwakumbuka Wenye Ulemavu

CRDB Lumumba, Yaadhimisha Siku ya Huduma kwa Wateja Kwa Kuwakumbuka Wenye Ulemavu
CRDB Bank Tawi la Lumumba, Yaadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja, kwa Kutembelea Kituo cha Watoto wenye ulemavu cha Jeshi la Wokovu, Kurasini jijini Dar es Salaam.. 
 Huku wakiongozwa na Mkurugenzi wa CRDB Tawi la Lumumba, John Almasi, wafanyakazi hao, walijumuika na watoto hao, kwa kuwapa zawadi mbalimbali, na kushiriki kutoa huduma mbalimbali shuleni hapo. 
 Akizungumzia siku hiyo, Mkurugenzi wa CRDB, Tawi la Lumumba, John Almasi, amesema wameamua kuwakumbuka watu wenye uhitaji, kwa vile CRDB ni Benki ya Jamii, na watu wenye uhitaji pia ni sehemu ya jamii, hivyo wameonelea ni bora waadhimishe, kwa kutembelea na kuwasawadia watoto wenye ulemavu wa kituo cha Jeshi la Wokovu, Kurasini. 
 Wakiishukuru benki hiyo, mwakilishi wa watoto hao, Mary Mwingira, aliishukuru Benki ya CRDB kwa kuwakumbuka na kuwajali, na akatoa wito kwa taasisi nyingine, ziige mfano wa CRDB kwa kuwakumbuka. 
 Makamo Mwenyekiti wa Chama cha Albino Tanzania, Joseph Masasi pia aliishukuru Benki ya CRDB kwa kuwakumbuka watu wenye ulemavu wa ngozi, na kukumbushia, watu hao wana changamoto za mahitaji ya ziada, yakiwemo mafuta mazito ya kuzuia miale ya jua. 
 Benki ya CRDB, imewakabidhi zawadi mbalimbali, watoto hao, vikiwemo vifaa vya shule na vyakula mbalimbali.
Mkurugenzi wa CRDB, Tawi la Lumumba, John Almasi akitoa zawadi kwa mmoja wa watoto wanaolelewa katika Kituo cha Watoto wenye ulemavu cha Jeshi la Wokovu, Kurasini jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni  Makamo Mwenyekiti wa Chama cha Albino Tanzania, Joseph Masasi na afisa wa kituo hicho

Mkurugenzi wa CRDB, Tawi la Lumumba, John Almasi akitoa zawadi kwa  watoto wanaolelewa katika Kituo cha Watoto wenye ulemavu cha Jeshi la Wokovu, Kurasini jijini Dar es Salaam. 
Mkurugenzi wa CRDB, Tawi la Lumumba, John Almasi akitoa zawadi kwa  watoto wanaolelewa katika Kituo cha Watoto wenye ulemavu cha Jeshi la Wokovu, Kurasini jijini Dar es Salaam. 
Wafanyakazi wa CRDB Tawi la Lumumba wakicheza na  watoto wanaolelewa katika Kituo cha Watoto wenye ulemavu cha Jeshi la Wokovu, Kurasini jijini Dar es Salaam. 
Wafanyakazi wa CRDB Tawi la Lumumba wakiwa na  watoto wanaolelewa katika Kituo cha Watoto wenye ulemavu cha Jeshi la Wokovu, Kurasini jijini Dar es Salaam. 
Picha ya pamnoja ya wafanyakazi wa CRDB Tawi la Lumumba wakicheza na  watoto wanaolelewa katika Kituo cha Watoto wenye ulemavu cha Jeshi la Wokovu, Kurasini jijini Dar es Salaam.