Tuesday, October 14, 2014

SHEREHE ZA NYERERE DAY ZAFANA SANA JIJINI LUSAKA, ZAMBIA



SHEREHE ZA NYERERE DAY ZAFANA SANA JIJINI LUSAKA, ZAMBIA
TAREHE 12/10/2014, UBALOZI WA TANZANIA NCHINI ZAMBIA UKISHIRIKIANA NA UONGOZI WA WATANZANIA WANAOISHI NA KUFANYA KAZI, BIASHARA NA KUSOMA NCHINI ZAMBIA ULIANDAA MICHEZO MBALIMBALI, CHAKULA NA VINYWAJI KATIKA KUSHEREHEKEA MAADHIMISHO YA SIKU YA KIFO CHA BABA WA TAIFA HAYATI MWALIMU JULIUS KAMBARAGE NYERERE (NYERERE DAY) INAYOANGUKIA TAREHE 14/10 KILA MWAKA. 
KATIKA MAADHIMISHO HAYO MICHEZO YA KUVUTA KAMBA, KUFUKUZA KUKU KWA AKINA MAMA, DRAFT, BAO NA MPIRA WA MIGUU ILIFANYIKA ILI KUMUENZI MWASISI WA UHURU NA TAIFA LA TANZANIA, KATIKA CHUO KIKUU CHA WAKATOLIKI – BONAVENTURE, LUSAKA. 
KATIKA CHUO HICHO KUNA WATANZANIA 25 WANAOCHUKUA MASOMO YA DIGRII YA KWANZA YA FILOSOFIA "PHILOSOPHY" AMBAO WALISHIRIKI KIKAMILIFU. TAZAMA PICHA MBALIMBALI ZA TUKIO HILO MUHIMU LA KUMUENZI MAREHEMU BABA WA TAIFA NCHINI ZAMBIA

.  SHEREHE HIZO ZILIZOFANA SANA ZILIHITIMISHWA KWA KUPATA VINYWAJI NA CHAKULA MAARUFU CHA KITANZANIA- PILAU UBALOZI – LUSAKA, ZAMBIA
MAANDALIZI YA SHEREHE
TIMU ZA KUVUTA KAMBA ZIKIPATA MAELEKEZO KABLA YA MCHEZO HUO KUANZA AMBAPO WACHEZAJII WA SIMBA WALISHINDA KWA AKINA DADA NA KAKA
TIMU ZA KUVUTA KAMBA ZIKIPATA MAELEKEZO KABLA YA MCHEZO HUO KUANZA AMBAPO WACHEZAJII WA SIMBA WALISHINDA KWA AKINA DADA NA KAKA
TIMU ZA SIMBA NA YANGA ZILITOKA SULUHU YA KUFUNGANA GOLI 1-1 KATIKA MPIRA WA MIGUU NA HIVYO KUSHINDWA KUTWAA KOMBE MAALUM LA NYERERE DAY. TIMU HIZO ZIMETAMBIANA KURUDIANA TENA ILI KUMPATA MSHINDI NA KUKABIDHIWA KOMBE KATIKA TAREHE ITAKAYOPANGWA NA KUKUBALIWA NA PANDE ZOTE ZINAZOHUSIKA.
SIMBA