Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Kisheria kutoka Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Bw. Nabor Assey akiongea na waandishi wa Habari (Hawapo pichani) kuhusu utekelezaji wa Miongozo ya Luanda inayohusu ukamataji na ushikiliaji wa watuhumiwa kabla ya kufunguliwa mashtaka itakayosaidia kupunguza mzigo kwa seriikali katika uendeshaji wa mahabusu na magereza yenye msongamano mwingi wa watuhumiwa na wafungwa, wakati wa Mkutano leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bi. Zamaradi Kawawa.