Afisa lishe wa Wilaya ya Njombe akitoa mada kwenye semina ya maafisa watendajji wa kata na viongozi wa vijiji wakati wa semina kuhusu kuongeza virutubishi kwenye vyakula iliyofanyika wilayani humo katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Njombe leo.Kampeni za matumizi ya vyakula vyenye virutubishi zinaendelea katika wilaya mbalimbali nchini.
Wanakijiji cha Ngalanga wilayani Njombe wakisikiliza mtaalamu wa lishe wa wilaya Bi Bertha Nyigu wakati wa semina juu ya matumizi ya vyakula vilivyoongezewa virutubishi iliyofanyika katika viwanja vya halmashauri ya wilaya ya Njombe.Kampeni za matumizi ya vyakula vyenye virutubishi zinaendelea katika wilaya mbalimbali chini ya usimamizi wa Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii na wadau wengine wa masuala ya afya.
Mtaalamu wa masuala ya lishe wa wilaya ya Njombe,Bi Bertha Nyigu, akijibu maswali ya wanavijiji mbalimbali waliofika kupata elimu ya masuala ya lishe na uongozeji virutubishi kwenye chakula.Kampeni za lishe bora na virutubishi zinaendelea kufanyika katika wilaya mbalimbali hapa nchini chini ya usimamizi wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.