Friday, September 12, 2014

NEWS ALERT: Moto wazuka tena katika Msikiti wa Mtambani leo




NEWS ALERT: Moto wazuka tena katika Msikiti wa Mtambani leo
Msikiti  wa  Mtambani uliopo Kinondoni jijini Dar es Saam uliungua kwa mara ya pili leo.  Msikiti huo ambao uliungua  mnamo Agosti 13, 2014 katika ghorofa yake ya juu na kuteketeza  eneo kubwa ambalo hadi sasa bado halijanza kufanyiwa  ukarabati.
Leo hii moto ambao inasemekana ulianza mmajira ya saa sita na nusu mchana   katika moja ya chumba ambacho wanafunzi wa kidato cha nne  wa kike wamekuwa wakipiga kambi ya kujisomea ikiwa ni katika maandalizi ya kukabiliana na mtihani wao wa taifa  utakaofanyika  baadaye mwaka huu.
 Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Kanda ya Kinondoni Camilius Wambura  amethibitisha jambo hilo na kusema kuwa hadi wanafika eneo la tukio chanzo bado hakijafahamika, na kwamba chumba ambacho moto ulianzia ni cha wasichana ambamo  magodoro manne yameungua.
"Katika janga la moto uliounguza madarasa  mwezi uliopita Jeshi la Polisi iliunda  timu ambayo ilikuwa ikichunguza chanzo cha moto huo hivyo na sasa timu hiyohiyo itaendele na uchunguzi wake kwa kuunganisha matukio haya mawili" alisema Wambura.
Wakizungumza bila ya kutaja majina yao kina mama wa msikitini hapo wao walisema  kwamba " sisi tulikuwa msikitini tunasoma qurani wakati tukivuta muda wa sala ya Ijumaa ndipo tuikasikia sauti za moto moto na kuona upande wa wanaume wakikimbia huku na kule kwa taharuki hivyo chanzo hasa cha moto sisi hatukijui.
Waumini wa msikiti huo walifanikiwa kuuzima moto huo na kusali swala ya Ijumaa kama kawaida.