mbunge wa Kalenga Godfrey Mgimwa akiongoza viongozi kutembelea ujenzi wa zahanati kijiji cha Mangalali |
Diwani wa kata ya Ulanda kulia akitoa ufafanuzi kwa mbunge wa jimbo la Kalenga Bw Mgimwa kuhusu maendeleo ya ujenzi wa zahanati kijiji cha Mangalali |
Katibu wa mbunge Mgimwa kulia Bw Martine Simangwa kulia akiteta jambo na mbunge Mgimwa. |
Mwananchi wa kijiji cha Mangalali akisalimia na mbunge wa jimbo la Kalenga Bw Godfrey Mgimwa |
Mbunge Mgimwa akidua sanjari na wananchi wa kijiji cha Mangalali |
Mmoja kati ya wananchi wa kijiji cha Mangalali akimpongeza mbunge Godfrey Mgimwa kwa utendaji kazi mzuri |
Katibu wa Mgimwa akiwaonya wana CCM wanaojipitisha jimboni kwa sasa |
Baadhi ya Wananchi wa kijiji cha Mangalali wakiwa katika mkutano wa mbunge wao Bw Mgimwa |
....................................................................................................... Na Matukiodaima.co.tz MBUNGE wa jimbo wa jimbo la Kalenga Godfrey Mgimwa ajipongeza kutumia kiasi cha zaidi ya Tsh milioni 68 kwa ajili ya kufanikisha utekelezaji wa ahadi zilizotolewa na mbunge aliyefariki Dr Wiliam Mgimwa kwa asilimia 90 kwa muda wa miezi mitatu pekee . Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mangalali baada ya kukamilisha ahadi ya bati 100 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya msingi Lukwambe , mbunge Mgimwa alisema kuwa alianza kutekeleza ahadi hizo hata kabla ya kuapishwa bungeni na hadi sasa bado asilimia 10 pekee ya utekelezaji wa ahadi zilizoachwa na mbunge aliyefariki dunia mwanzoni mwa mwaka huu marehemu Dr Mgimwa ambae alikuwa ni babake mzazi. " Ni jambo la kumshukuru mwenyezi Mungu kwani ahadi zilizokuwa zimetolewa na mbunge aliyefariki dunia marehemu Dr wiliam Mgimwa zilikuwa ni asilimia 100 na hadi mnanichangua kuwa mbunge ahadi hizo zilikuwa bado kutekelezwa na ndio sababu ya mimi katika kampeni kutoahidi ahadi mpya zaidi ya kuzipokea zile zilizoachwa na baba ambazo kimsingi nilizipokea .......ila kwa sasa ahadi hizo nimetekeleza kwa asilimia 90 bado asilimia 10 pekee ambazo hadi mwakani nitakuwa nimezimaliza kikubwa naomba mzidi kuniombea uzima" alisema mbunge Mgimwa. Alisema kuwa hakuweza kuahidi ahadi mpya wakati wa kampeni hizo za uchaguzi mdogo jimboni humo kutokana na kuwepo kwa ahadi nyingi ambazo zilikuwa zimetolewa na mbunge aliyepita na zilikuwa bado kutekelezwa na muda wa utekelezaji ulikuwa bado hivyo aliamua kuzichukua zote kama zilivyo na kuanza kuzifanyia kazi moja baada ya nyingine . Mbunge Mgimwa alisema kuwa ahadi hizo zinazotekelezwa ni zile ahadi binafsi ambazo mbunge aliyepita alikuwa amezitoa ila zipo ahadi mbali mbali ambazo zimo katika ilani ya CCM ambazo pia zimeendelea kutekelezwa kwa nguvu kubwa . Hata hivyo alisema kuwa ahadi ambazo zimetekelezwa kwa asilimia 90 ambazo zilikuwa ni ahadi binafsi ni pamoja na elimu ,afya na uchangiaji wa vikundi vya Vicoba pamoja na uanzishwaji wa vikundi hivyo pia katika sekta ya michezo na huduma nyingine za kijamii kama upelekaji wa umeme katika maeneo ya kata ya Mgama na Magulilwa zoezi hilo linaendelea ambayo ahadi hiyo ya umeme ipo katika ilani ya CCM pamoja na zile za huduma za maji vijijini ambazo baadhi ya maeneo mradi kata ya Maboga na kata ya Lumuli wa maji unatekelezwa . Pia alisema kuwa bado anautamani ubunge wa jimbo hilo la Kalenga kwa mwaka 2015 -2020 hivyo kamwe hatawaangusha wana Kalenga kwa kipindi hiki cha miaka miwili alichopewa hadi 2010. " Ndugu zangu hii nafasi ya ubunge mimi nimeipata mwishoni ila sikutaka kuwaangusha nilitaka kuwaonyesha utendaji wangu na kamwe sitakuwa mbali na ninyi wananchi wangu nitakuwa bega kwa bega kuhakikisha jimbo la Kalenga linapata maendeleo na linakuwa ni jimbo la mfano katika maendeleo kule bungeni kutokana na umri wangu wabunge wananiita bwana mdogo ila kiutendaji kweli ni bwana mkubwa kwani kati ya wabunge zaidi ya 300 bungeni mimi ni mmoja kati ya wabunge tuliochanguliwa kuingia katika kamati ya bunge ya bajeti ya serikali " alisema mbunge Mgimwa . Awali katibu wa mbunge huyo Martine Simangwa aliwaonya wana CCM ambao wameendelea kujipitisha katika jimbo hilo na kuwa kwa kufanya hivyo ni kutowatendea haki wananchi wa jimbo la Kalenga ambao kwa sasa wameshikamana na wapo tayari kuona maendeleo na sio kampeni za uchaguzi wa mwaka 2010. " wapo baadhi ya wana CCM bila haya wameendelea kujipitisha kwa wananchi na kuponda utendaji huu mzuri wa mbunge Godfrey Mgimwa ....sasa wananchi nawaombeni sana msidanganyike na watu hao kwa sasa mbunge ni Godfrey Mgimwa wakija na kuwapa pesa chukueni ila msikubali kugawanywa kwa misingi ya pesa kubalini kuungana katika misingi ya kimaendeleo" Kwa upande wao wananchi hao walieleza kufurahishwa na utendaji mzuri wa mbunge wao Mgimwa na kuwa kamwe hawatakubali kudanganyika na kuwa wamejipanga kumchukulia fomu mwakani ili kuwaongoza vipindi vingine viwili zaidi baada ya kuona utendaji wake mzuri. MWISHO |