Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni za wastaafu PPF, Bw.William Erio ameipongeza benki ya CRDB kwa kuendelea kuwa benki bora yenye huduma nzuri zaidi hapa nchini.
Bw. Erio aliyasema hayo jijini Arusha katika hafla ya chakula cha jioni kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu wa PPF iliyofanyika katika hoteli ya Naura Springs.
Mkurugenzi huyo alisema kuwa Shirika lake lina faraja kubwa kuona benki ya CRDB ambayo PPF ni mmoja ya wanahisa wake wakuu, ikiendelea vizuri na kufikia viwango vya kimataifa. Bwana Erio aliendelea kuwahimiza wastaafu na watanzania wote kwa ujumla kutumia huduma za benki ya CRDB kwani zimeundwa kukidhi mahitaji halisi wa watanzania.
Mkurugenzi Mkuu wa PPF, William Eriyo akizungumza na wageni waalikwa katika hafla ya chakula cha jioni kilichoandaliwa na Benki ya CRDB kwa ajili ya wajumbe wa mkutano Mkuu wa PPF katika hoteli ya Naura Springs jijini Arusha. Kushoto ni Meneja Mahusiano wa Benki ya CRDB, Godwin Semunyu. (Na Mpiga Picha Wetu)
Mkurugenzi Mkuu wa PPF Bwana William Erio (kushoto), akiwa pamoja na Mkurugenzi wa Uendeshaji wa NSSF, Crescentius Magori na Meneja Mahusiano wa Benki ya CRDB, Godwin Semunyu (kulia), katika hafla ya chakula cha jioni kwa wajumbe wa mkutano Mkuu wa PPF iiyoandaliwa na benki ya CRDB katika hoteli ya Naura Springs jijini Arusha.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB Bw.Martin Mmari (Kulia) ambaye pia ni Mkurugenzi wa Fedha wa PPF akifuatilia jambo katika hafla hiyo.