Thursday, September 04, 2014

Benki ya BOA kuwawezesha wasambazaji wa bidhaa za Vodacom



Benki ya BOA kuwawezesha wasambazaji wa bidhaa za Vodacom
 Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Rene Meza (kulia) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akizindua ushirikiano wa kampuni yake na Benki ya Afrika (BOA) Tanzania unaowawezesha mawakala wa M-pesa na wasambazaji wa huduma za Vodacom kupata miko nafuu na bila dhamana kuinuua biashara zao. Kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya BOA, Ammish Owusu – Amoah.Hafal hiyo imefanyika Makao Mkauu ya Vodacom, Dar es salaam.
 Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Afrika (BOA) Tanzania Ammish Owusu – Amoah (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Rene Meza wakipongezana mara baada ya kutangaza rasmi ushirikiano unaowawezesha mawakala wa M-pesa na wasambazaji wa huduma za Vodacoyam kupata mikopo nafuu na bila dhamana kutoka BOA kwa lengo la kuinuua biashara zao. Mikopo hiyo ni kati ya Sh 10 Milioni na 75 Milioni.
 Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Afrika (BOA), Ammish Owusu – Amoah(kushoto)akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari(hawapo pichani)kuhusiana na kuingia ubia na Vodacom Tanzania ambao utawawezesha mawakala wa kuuza na kusambaza bidhaa za kampuni hiyo kupata mikopo ya masharti nafuu na bila amana ili kuwawezesha kutoa huduma bora kwa wateja wao,kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania,Rene Meza.
 Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya Afrika (BOA)-Tanzania na wa Vodacom Tanzania wakifuatilia  mkutano wa waandishi wa habari kuhusiana na uzinduzi wa ushirikiano kati ya BOA benki na  Vodacom Tanzania  ambao utawawezesha mawakala wa M-pesa na wauzaji wakubwa wa bidhaa za Vodacom kupata mikopo ya kati ya Sh 10 Milioni na 75 Milioni kwa masharti nafuu na bila amana ili kuwawezesha kutoa huduma bora kwa wateja.
Ofisa Mkuu wa Mauzo na Usambazaji wa Vodacom Tanzania,Hassan Saleh(kulia) na Mkuu wa Mauzo  wa M pesa Franklin Bagala wakifuatilia  mkutano wa waandishi wa habari kuhusiana na uzinduzi wa ushirikiano kati ya BOA benki na  Vodacom Tanzania  ambao utawawezesha mawakala wa M-pesa na wauzaji wakubwa wa bidhaa za Vodacom kupata mikopo ya kati ya Sh 10 Milioni na 75 Milioni kwa masharti nafuu na bila amana ili kuwawezesha kutoa huduma bora kwa wateja.