Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania ,Kelvin Twissa akitoa mada juu ya huduma zinazotolewa na kampuni yake wakati wa Warsha ya kushirikishana uzoefu kuhusu njia za kuboresha na kupanua huduma za kifedha kwa biashara ndogo na za kati hapo jana. Warsha hiyo iliandaliwa na Tanzania Private Sector Foundation (TPSF) na kudhaminiwa na Vodacom.Kushoto ni muongozaji wa mada Felix Mlaki na Katikati ni Mtaalamu toka Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE)Moreme Marwa.
Mmoja wa washiriki wa Warsha ya kushirikishana uzoefu kuhusiana na njia za kuboresha na kupanua huduma za kifedha kwa biashara ndogo na za kati iliyoandaliwa na Tanzania Private Sector Foundation (TPSF) na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania, akisoma moja ya jarida la Vodacom wakati wa warsha hiyo iliyofanyika kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam hapo jana.
Baadhi ya washiriki wa Warsha ya kushirikishana uzoefu kuhusu njia za kuboresha na kupanua huduma za kifedha kwa biashara ndogo na za kati iliyoandaliwa na Tanzania Private Sector Foundation (TPSF) na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania,wakifuatilia mada kwa makini zilizokuwa zikitolewa wakati wa warsha hiyo iliyofanyika kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam hapo jana.