Wednesday, August 20, 2014

Airtel yawafikishia Wanakijiji wa Sigunga Kigoma huduma za mawasiliano



Airtel yawafikishia Wanakijiji wa Sigunga Kigoma huduma za mawasiliano
 Timu ya Airtel wakiongozwa na Emanuel Rafael zone Businnes Manager mara baada ya uzinduzi wa mnara wa kampuni ya mawasiliano ya airtel katika kijiji cha Sigunga wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma hafla ya uzinduzi imefanyika jana kijijini humo
 Mkuu wa wilaya Khadija Nyembo akiongea wakati wa uzinduzi wa mnara wa airtel katika kijiji cha Sigunga wilaya ya Uvinza mkoani kigoma hafla ya uzinduzi imefanyika jana kijijini humi
 Kikundi cha Ngoma kikiburudisha katika sherehe za uzinduzi wa mnara wa Airtel kijiji SIGUNGA wilaya ya Uvinza mkoani  Kigoma.
=======  =======  =========
Airtel yawafikishia Wanakijiji wa Sigunga Kigoma huduma za mawasiliano
·         Yazindua mnara wa mawasiliano katika kijiji cha Sigunga mkoani Kigoma, wanakijiji Kunufaidika na huduma za mawasiliano ya simu za mkononi toka Airtel
Kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel leo imezindua rasmi huduma za mawasiliano katika kijiji cha Sigunga wilaya ya  Uvinza mkoani Kigoma

Uzinduzi huo unafatia jitihada za kampuni ya Airtel kuendelea kuboresha mawasiliano ya huduma za simu za mkononi katika maeneo mbalimbali nchini husasani katika maeneo ya vijijini huku lengo likiwa ni kuzifikia jamii zinayoishi pembezoni mwa nchi huduma bora ya Airtel Money.

Akiongea wakati wa uzinduzi wa huduma za mawasiliano Sigunga,  Meneja Mauzo kanda ya Ziwa bwana Raphael Daudi alisema " Airtel inatambua adha wanayoipata wakazi wa kijiji cha Sigunga na maeneo ya jirani katika kupata huduma za mawasiliano kwa muda mrefu sasa,  hivyo tumeonelea ni vyema basi tukachukua hatua ya kuboresha huduma hizi muhimu kwa kuwafikishia wanakijiji hawa  mawasiliano yatakayowawezesha kufanya shughuli zao za kila siku kwa ufanisi zaidi

Kupitia mnara huu sasa tunaweza kuwaunganisha wanakijiji hawa na maeneo mengine ya nchi, tutawawezesha kupata masoko ya kuuza biashara zao kwa urahisi, tumewawezesha kupata huduma za kifedha kupitia huduma yetu ya Airtel Money ambapo sasa wataweza kupokea na kutuma pesa kwa ndugu jamaa na marafiki pia kupokea malipo ya biashara zao na kuweza kufanya malipo mbalimbali ya huduma muhimu wakiwa majumbani mwao. Sambamba na hilo mawasiliano jijini hapa yamekuwa chachu ya maendeleo na ukuaji wa shughuli za kiuchumi kwa ujumla.

Kwa upande mkuu wa wilaya ya Uvinza Khadija Nyembo alisema" Tunawashukuru sana Airtel kwakutambua kwa vitendo umuhimu wa mawasiliano kwa kutufikishia mawasiliano kijijini hapa. Kupitia mawasiliano ya Airtel tumeweza kuboresha usalama wa raia na mali zao, kuwezesha kufanyika kwa  shughuli za kiuchumi kiufani , wakulima sasa wanauhakika wa kupata masoko na kupata malipo kwa kupitia simu ya mkonono.  sambamba na hilo mawasiliano hayo yamewezesha huduma muhimu za  kijamii kuboreshwa zaidi.

Natoa wito kwa wakazi wa Sigunga Na vijiji vya jirani kutumia mawasiliano haya katika kukuza uchumi wao na wa jamii kwa ujumla.

Wakiongea kwa wakati tofauti wakazi wa Sigunga wameishukuru Airtel kwa kuwafikishia  mawasiliano hayo nakusema , tumekuwa na adha kubwa ya huduma za simu kabla ya mawasiliano haya kufikishwa kijijini hapa lakini kwa sasa kero hiyo imekwisha kabisa hivyo tunaipongeza sana kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa juhudi zao.