Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), Bibi Jacqueline Mneney Maleko akipokea Kompyuta, Vifaa vya Ofisi na Samani kutoka kwa Mwakilishi wa Taasisi ya Marekani ya USAID - East Africa Trade Hub,Bw. Peter Nash. Vifaa hivi ni kwa ajili ya kuanzisha rasmi Ofisi za Kamati za Ushirikiano Mipakani (Joint Border Committees) zilizoanzishwa kwenye mipaka 7 ambayo ni Namanga, Kasumulu, Tunduma, Rusumo, Kabanga, Mtukula na Sirari. Madhumuni yake ni kuimarisha ufanisi wa kupitisha mizigo mipakani na kupata taarifa za biashara mipakani. Tukio hili lilifanyika tarehe 19 Agosti 2014 katika Uwanja wa Mwl. J.K.Nyerere Barabara ya Kilwa, Dar-es-Salaam. Wanaoshuhudia ni Maafisa Waandamizi na Watendaji wa TanTrade. (Picha na TanTrade)