Kikosi cha Timu Ya Survey wakiwa katika picha ya pamoja.
Wachezaji wa Survey Veterani wakiwa katika picha yapamoja Wachezaji wa Coastal U 20 kabla ya mechi.
Mchezaji wa Timu ya Survey Veterani Hamad Shaweji
akimtoka mchezaji wa Coastal Union U 20 katika mashindano ya kilele cha nane nanae yaiyofanyika viwanja vya mkwakwani Jijini Tanga.
NA ELIZABETH KILINDI, TANGA
TIMU ya Survey Veteran ya jijini Dar es Salaamu, Jumapili iliyopita ilivuna sare ya bao 1-1 dhidi ya kikosi cha vijana wa chini ya miaka 20 wa timu ya Coastal Union katika mechi ya kirafiki iliyochezwa Uwanja wa Mkwakwani, jijini Tanga.
Ikiwa ni mechi ya pili kwa Survey katika ziara yao ya jijini hapa, baada ya kuwafunga Veterani Kombaini ya Tanga 2-1 katika mechi yao ya kwanza dhidi ya Kombaini ya Maveterani wa hapa, licha ya kutoka sare walicheza soka ya kueleweka.
Mechi hiyo iliyofanyika chini ya udhamini wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), katika kuadhimisha kilele cha wakulima maarufu kama Nane Nane, imeacha gunzo kubwa kwa wapenzi na mashabiki wa soka.
Mechi hiyo ya Jumapili iliyochezwa katika uwanja wa Mkwakwani, jijini hapa, bao la Survey lilifungwa na Moses Mdamo katika dakika ya 20 kabla ya vijana wa Coastal Union kusawazisha dakika ya 40, likifungwa na Kapamba Kibadeni.
Baada ya filimbi ya mwisho, Kocha Seleman Mgaya ambaye pia ni Katibu wa timu ya Survey Veteran, alisema wamefurahia ushirikiano wa NSSF hasa kuonyesha mchango wao katika kusaidia michezo.
"Tunaishukuru NSSF kwa moyo wa kutukutanisha kimichezo kwani wameonyesha kututambua. Kwetu hili ni jambo la kujivunia, tunaahidi kuwa tayari kutoa kila aina ya ushirikiano kwao," alisema Mgaya.