Mkurugenzi Mtendaji wa SOS Children Tanzania, Anatory Rugaikamu (katikati) akiongea na waandishi wa habari leo katika Hoteli ya Serena wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya Kuchangisha Pesa kwaajili ya Kuwasaidia Watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu, Kampeni hiyo inafanywa na SOS Children kwa kushirikiana na Kampuni ya Montage Ltd.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Montage Ltd, Bi Teddy Mapunda akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya Kuchangisha fedhaa kwa ajili ya kuwasaidia watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu. Kampeni hiyo inafanywa na SOS Children kwa kushirikiana na Kampuni ya Montage Ltd.
Baadhi ya waandishi wa Habari wakiwa Katika mkutano huo uliofanyika katika hotel ya Serena mapema leo.