Mkuu wa Wilaya ya Same Bw. Herman Kapufi akisisitiza jambo juu ya Mafunzo ya Mradi wa kuijengea Jamii Uwezo Wa Kupunguza Athari Za Maafa katika Wilaya yake wakati timu ya Wataalam Kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania na Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika walipo mtembelea Ofsini kwake kabla ya kuanza mafunzo hayo leo, Hedaru Wilayani Same.
Mratibu kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu wa Mradi Wa Kuijengea Jamii Uwezo wa kupunguza Athari Za Maafa kwa Mikoa iliyoathirika zaidi na Ukame Bw. Harrison Chinyuka akisitiza umuhimu wa Mafunzo ya Utekelezaji wa Mradi huo kwa Wataalam wa kutoka kata za Hedaru, Makanya na Vunta (hawapo pichani) wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo leo, Hedaru, Wilayani Same (katikati) Afisa Mtendaji Kata Hedaru, Bw. Jackson Mbwambo (kushoto) Mratibu Maafa Wilaya, Same, Bw. Ally Mngwaya.
Baadhi ya Wataalam katika Sekta ya Kilimo, Mifugo, Afya, Elimu na Utawala wa kata ya Hedaru, Makanya na Vunta wakiwa katika majadiliano ya jinsi ya kutekeleza Mradi Wa Kuijengea Jamii Uwezo wa kupunguza Athari Za Maafa katika kata zao leo , Hedaru Wilayani Same.