Tuesday, August 26, 2014

MWENGE WA UHURU WAPOKELEWA MKOANI MANYARA




MWENGE WA UHURU WAPOKELEWA MKOANI MANYARA
Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Elaston Mbwilo (kushoto) akijiandaa kupokea mwenge wa uhuru kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Laurence Gama kwenye Kijiji cha Msitu wa Tembo Wilayani Simanjiro jana, ambapo kwenye Mkoa wa Manyara, Mwenge wa Uhuru unatarajia kutembelea miradi 56 yenye thamani ya shilingi bilioni 4.3.
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru, Rachel Kassanda akikagua shamba darasa la vitunguu la mkulima Charles John Msangi wa Kijiji cha Lemkuna, mara baada ya mwenge kuingia Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara jana,mkulima huyo alitumia sh3 milioni kuliandaa na anatarajia kupata mavuno yenye thamani ya zaidi ya sh10 milioni.
Watoto wa Kijiji cha Msitu wa Tembo, Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, wakishangilia kwa kutumia majani mara baada ya mwenge wa uhuru kuingia kwenye kijiji chao juzi ukitokea Mkoani Kilimanjaro, ambapo ukiwa mkoani huo unatarajia kutembelea miradi 52 yenye thamani ya sh4.3 bilioni.