Balozi Mdogo wa Tanzania-Dubai, Mhe. Omar Mjenga akiwa katika picha ya pamoja na watendaji wakuu wa benki ya UBL ya Dubai, Bw. Shaikh Muhammad Liaque, Makamu wa Rais wa UBL (kushoto) na Bw. Syed Abbas Bokhari walipomtembelea ofisini kwake leo.
Wakiwa katika mazungumzo, ambapo Mhe. Mjenga amewaomba kuangalia uwezekano wa kuajiri Watanzania kwenye Benki hiyo kuja kufanya kazi Dubai. Mwaka jana, UBL ilifungua ofisi ya Dar es Salaam kuwa ofisi ya Kanda ya Afrika. Aidha,wamegusia suala la kufungua matawi zaidi Arusha, Moshi, Mwanza, Mbeyana Matawi mengine zaidi Jijini Dar es salaam. Hii yote itafanikisha kuongeza nafasi za ajira kwa Watanzania.