Thursday, August 21, 2014

Mamlaka ya Elimu Tanzania inatarajia kukabidhi madawati 2000 kwa shule za Msingi 10



Mamlaka ya Elimu Tanzania inatarajia kukabidhi madawati 2000 kwa shule za Msingi 10
Meneja Habari, Elimu na Mawasiliano toka Mamlaka ya Elimu Tanzania Bi Sylvia Lupembe akiongea na waandishi wa habari (Hawapo pichani) kuhusu jitihada wanazofanya kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ili kukabiliana na changamoto katika sekta ya elimu,wakati wa mkutano uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Mkuu wa kitengo cha Masoko na Uhusiano toka benki ya KCB Bi. Christina Manyenye.
Meneja Sheria na Uhusiano toka kampuni ya uuzaji na usambazaji wa mafuta ya TOTAL Bi. Masha Msuya Akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu mpango wao wa kutoa zaidi ya madawati 1000 kwa kushirikiana na wadau wengine , mpango huu utaanza kutekelezwa kwa kuanzia na mkoa wa Dar es Salaam.kulia ni Mkuu wa kitengo cha Masoko na Uhusiano toka benki ya KCB Bi. Christina Manyenye.
Afisa Rasilimali Fedha toka taasisi isiyo ya kiserikali ya Social Action Trust Fund (SATF) Bw. Timotheo Tenga akiwaeleza jambo waandishi wa habari( hawapo pichani) wakati wa mkutano uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Meneja Sheria na Uhusiano toka kampuni ya uuzaji na usambazaji wa mafuta ya TOTAL Bi. Masha Msuya.
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo wakiwasikiliza wawasilishaji toka Mamlaka ya Elimu Tanzania, KCB, TOTAL, Social Action Trust Fund (SATF) leo Jijini Dar es Salaam. PICHA NA HASSAN SILAYO-MAELEZO