Saturday, August 09, 2014

MAGUFULI AKAGUA UJENZI WA KIVUKO CHA MSANGAMKUU (MV. MTWARA), DARAJA LA KIGAMBONI PAMOJA NA UKARABATI WA KIVUKO CHA MV. KIGAMBONI


MAGUFULI AKAGUA UJENZI WA KIVUKO CHA MSANGAMKUU (MV. MTWARA), DARAJA LA KIGAMBONI PAMOJA NA UKARABATI WA KIVUKO CHA MV. KIGAMBONI
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli leo amefanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Daraja la Kigamboni ambalo ujenzi wake utakamilka ifikapo Juni mwaka 2015.

Awali, Dkt.Magufuli alianza kwa kukagua ujenzi wa kivuko kipya cha Msanga Mkuu maeneo ya Kurasini, kivuko hiki kinajengwa na mkandarasi mzalendo na kitakamilika ndani ya kipindi cha miezi miwili.

Aidha, Waziri wa Ujenzi amefanya ukaguzi wa ukarabati wa matengenezo makubwa ya kivuko cha MV.Kigamboni huko Kigamboni, ukarabati huo unafanywa na Wakandarasi Wazalendo kutoka Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania - Kamandi ya Jeshi la Majini. 

Kivuko cha MV.Kigamboni kilijengwa mwaka 2009 na kwa taratibu za vivuko vinavyofanya safari zake katika maji ya chumvi hutakiwa kufanyiwa ukarabati mkubwa kila baada ya miaka mitano. 

Hata hivyo, Dkt.Magufuli amewahakikishai wananchi wa Kigamboni kuwa mwaka wa fedha 2014/15 Serikali imetenga kiasi cha shilingi bilioni 3.7 kwa ajili ya kununua kivuko kipya kitakachofanya safari zake maeneo ya Kigamboni.

Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli wa kwanza kulia akipewa maelezo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mhandisi Mussa Iyombe kuhusu ujenzi wa kivuko cha Msanga Mkuu(MV Mtwara) kilicho katika hatua za mwisho za matengenezo chini ya Kampuni ya Sangoro Marine Transpot Limited. 

Luteni Kanali Abel Gwanafyo akitoa maelezo kwa Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kuhusu ukarabati wa Kivuko cha MV. Kigamboni kinachofanyiwa ukarabati na Jeshi la Wananchi wa Tanzania kupitia kikosi cha Wanamaji (Nav) Kigamboni jijini Dar es Salaam. 

Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akitoka katika kivuko cha MV. Kigamboni mara baada ya Ukaguzi.