Saturday, August 02, 2014

kilio cha mdau juu ya hali ya uchafuzi wa Mazingira



kilio cha mdau juu ya hali ya uchafuzi wa Mazingira
Naomba kutoa pendekezo kwa Wizara husika,Wakuu wa mikoa ,Wakuu wa wilaya , Mameya na Halimashauri husika juu ya uchafu unaozidi kukidhili kila siku kwa baadhi ya maeneo ya miji mikuu na karibu na mahoteli yanayolisha wasafiri kuelekea mikoani, nadhani na wao pia watakuwa mashaidi juu ya mifuko ya plastic inayozagaa ovyo barabarani, na mitaro ya maji iliyojaa mifuko na maji machafu, na mchanga iliyoachwa baada ya kuziburiwa katika mitaro,

Ombi langu kwa 

Serikali itoe ajira kwa vijana wasio na kazi kuokota uchafu kila siku hata kwa masaa mawili kila siku kwa kuwalipa pesa kidogo na pia wawape jukumu la kuwakamata wahusika wanaotupa uchafu hovyo ili walipishwe faini, na kila kijana atakaye kamata mtu akitupa uchafu pesa atakayomtoza iwe yake ya mfukoni kuwapa motisha kujitolea kuwadhibiti wanaotupa hovyo uchafu, na kwa upande wa mabasi waweke ndoo ya kukusanyia uchafu kwenye mabasi yote hata kama ni daladala, na waandike matangazo ya kutotupa uchau nje ya gari au basi.  mimi nahisi kila mtu akiwa anadhamana ya kumkamata mtu na kumlipisha faini itasaidia sana maana kila mtu atakuwa akimuogopa mwengine,

na kwa wazizi au walezi tuwafundishe watoto wetu tokea wadogo kutotupa uchafu ovyo,

Huu ndiyo mtazamo wangu natumaini wengi watakuwa na mtazamo tofauti na maoni yao tofauti, karibuni kwa kuchangia

Mdau anaekerwa na Uchafuzi wa Mazingira.