Saturday, August 23, 2014

HARUSI YA MWIMBAJI WA KWETU PAZURI NA MTANZANIA




SHANGWE ZA GK: HARUSI YA MWIMBAJI WA KWETU PAZURI NA MTANZANIA Jumapili iliyopita ya tarehe 17 Augusti 2014 katika kanisa la Wasabato la Ushindi SDA lililopo Mikocheni jijini Dar es salaam kulishuhudiwa wapendanao wawili Warren Bright pamoja na Claire Humure kutoka nchini Rwanda wakihitimisha safari yao ya uchumba na kuwa mume na mke rasmi kwa ibada ya ndoa takatifu iliyofungwa kanisani hapo.

Ibada hiyo ilihudhuriwa na ndugu, jamaa na marafiki wakiwemo baadhi ya waimbaji wa kwaya ya Ambassadors of Christ ya Rwanda ambao bibi harusi ni mwimbaji wao wa sauti ya kwanza. lakini pia kama haitoshi wapambe wa kuu wa maharusi hao ama wasimamizi pia ni waimbaji wa kwaya hiyo almaarufu kama Kwetu pazuri. GK inawatakia maisha mema na marefu ya ndoa maharusi hao.

Claire akiwa mwenye furaha kuelekea ibadani tayari kwa ndoa.
Claire pamoja na kaka yake wakiingia kanisani.
Maharusi wakiwa wameambatana pamoja.
Claire akimnong'oneza jambo mumewe.
Flora pamoja na Eric wapambe wa maharusi wakiwa makini.
Waimbaji wa Ambassadors kutoka Rwanda wakiwa na nyuso za furaha.
Ni furaha tuu ilitawala.
Ilikuwa wakati mzuri wa kuimba.
Safii unaweza kukisia wimbo uliokuwa ukiimbwa.
Harusi ilipendeza sana.
Malkia wa Kwetu Pazuri Yvonne Umulisa aliyevaa kitenge akiwapongeza maharusi mara baada ya harusi yao ya kimila iliyofanyika Rwanda.
Maharusi na wapambe wao katika picha ya pamoja. ©AOCC na Kj Marcello.