Wednesday, August 06, 2014

BANDA LA OFISI YA WAZIRI MKUU LAVUTIA NANE NANE DODOMA




BANDA LA OFISI YA WAZIRI MKUU LAVUTIA NANE NANE DODOMA
Baadhi ya Wananchi wa Mjini Dodoma wakipata maelezo ya Uwekezaji na Uwezeshaji kutoka kwa Mchumi Mwandamizi wa Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Vedasto Manumbu walipotembelelea Banda la Ofisi ya Waziri Mkuu katika Maonesho ya Nane Nane yanayoendelea Mjini Dodoma, Viwanja vya Nzuguni.
Mratibu wa Shughuli za Serikali Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Mollay akifafanua uratibu wa shughuli za serikali kwa Wanafunzi Shule ya Msingi Nzuguni "B" walipotembelea Banda la Ofisi ya Waziri Mkuu katika Maonesho ya Nane Nane yanayoendelea Mjini Dodoma, Viwanja vya Nzuguni.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Nzuguni "B" wakisoma Picha zenye historia za Mawaziri Wakuu Wastaafu wa Tanzania, zilizopo katika Banda la Ofisi ya Waziri Mkuu katika Maonesho ya Nane Nane yanayoendelea Mjini Dodoma, Viwanja vya Nzuguni.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)