Jaja                akipokea nakala ya mkataba wake kutoka kwa Katibu Mkuu wa                Young Africans Bw Beno Njovu leo maraa baada ya kusaini                kuitumikia kwa miaka miwili
        Hatimaye mshamabuliaji Geilson Santos Santana "Jaja" raia wa Brazil leo amesaini mkataba wa miaka miwili (2014-2016) kuitumikia timu ya Young Africans kwa ajili ya michuano mbalimbali ikiwemo ya Ligi Kuu ya Vodacom pamoja na mashindano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika mwakani.
Katibu mkuu wa Young              Africans  Bw Beno Njovu amesema usajli wa Jaja unakua ni wa              pili msimu huu kwa wachezaji wa kimataifa baada ya awali              kumsajili kiungo mshambuliaji Andrey Coutinho ambaye pia ni              raia wa Brazil.
        "Kazi              yetu uongozi ni kutekeleza maelekezo ya kocha mkuu pamoja na              benchi la ufundi, walitoa mapendekezo ya usajili kabla              hawajaanza kazi na mengine baada kuwasili yote tunajitahidi              kuyatekeleza ili kila kitu kiende safi" alisema Beno.
          Jaja ambaye alizaliwa              tarehe 21 Septemba 1985 na kukulia katika mji wa Aracaju              nchini Brazili mpaka anasajiliwa na timu ya Young Africans              alikuwa akiichezea timu ya Itabaina FC iliyopo nchini              Brazil.
        Mshambuliaji huyo mwenye              mwili uliojaa vizuri tayari alishaanza mazoezi tangu              katikati ya wiki iliyopita chini ya Kocha Mkuu Marcio Maximo              na msaidizi wake Leonado Neiva ambao wanaendelea kukinoa              kikosi cha Young Africans kwa ajili ya michuano mbalimbali.
         
