Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Maxcom Africa Limited, Bwa.Ahmed Salum Lussasi akielezea namna mashine ya MaxMalipo inavyoweza kufanya kazi katika suala zima la jamii kujikwamua na umaskini,ikiwemo hasa kwa wajasiliamali mbalimbali,kwenye maonyesho ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea kwenye uwanja wa maonyesho wa Mwalimu Nyerere mjini Dar es salaam ambapo Waziri Mkuu Mh Mizengo Pinda alipita kujionea huduma mbalimbali zitolewazo na kampuni hiyo.
Waziri Mkuu Pinda,akisalimiana na baadhi ya Wafanyakazi wa kanpuni ya Maxcom Africa Limited ,alipowatembelea kwenye banda lao mapema leo mchana,kwenye maonyesho ya Biashara ya 38 ya Kimataifa yanayoendelea kwenye uwanja wa maonyesho wa Mwalimu Nyerere mjini Dar es salaam
Waziri Mkuu Pinda,akimueleza jambo Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Maxcom Africa Limited, Bwa.Ahmed Salum Lussasi,alipotembelea banda la kampuni hiyo mapema leo mchana,kwenye maonyesho ya biashara ya 38 ya Kimataifa yanayoendelea kwenye uwanja wa maonyesho wa Mwalimu Nyerere mjini Dar es salaam.