Monday, July 07, 2014

VODACOM FOUNDATION YAFUTURISHA WATOTO YATIMA ZANZIBAR



VODACOM FOUNDATION YAFUTURISHA WATOTO YATIMA ZANZIBAR
Mgeni rasmi kwenye hafla ya kufuturisha watoto waishio katika mazingira magumu mjini Zanzibar,Kadhi Mkuu wa Zanzibar,akiwasili kwenye hafla hiyo iliyoandaliwa na Vodacom Foundation na kupokewa na Meneja wa Vodacom tawi la Zanzibar, Mohamed Mansoor.
Baadhi ya watoto wanaoishi katika mazingira magumu mjini Zanzibar wakimsikiliza Kadhi Mkuu Zanzibar Khamis Haj alipokuwa anazungumza nao wakati wa hafla ya kufuturisha watoto hao iliyoandaliwa na Vodacom Foundation jana.
Kadhi Mkuu wa Zanzibar akikabidhi vyakula,mbuzi, mafuta, mchele na madaftari kwa watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi mjini Zanzibar kwa niaba ya Vodacom Foundation,Wakati wa hafla ya kufuturu hapo jana,Anaeshuhudia kushoto ni Meneja wa Vodacom Tanzania tawi la Zanzibar Mohamed Mansoor.
Viongozi wa dini mjini Zanzibar pamoja na wa Vodacom Tanzania wakiongozwa na mgeni rasmi Kadhi wa Zanzibar Khamis Haj wakipata futari katika hafla hiyo iliyoandaliwa na Vodacom Foundation kwaajili ya watoto waishio katika mazingira hatarishi mjini Zanzibar.
Kadhi Mkuu wa Zanzibar, Khamis Haj akihutubia kwenye hafla ya kufuturisha watoto wanaoishi katika mazingira magumu mjini Zanzibar,Hafla hiyo iliandaliwa na Vodacom Foundation.
Juma Haji mkazi wa Zanzibar akisaidia kuwagawia Maji na vyakula baadhi ya watoto waishio katika mazingira magumu waliohudhuria hafla ya kufuturu iliyoandaliwa na Vodacom Foundation kwaajili yao hapo jana.