UFARANSA imekuwa timu ya kwanza kuaga kombe la dunia kwenye hatua ya robo fainali baada ya kufungwa 1-0 na Ujerumani.
Kwa ushindi huu, Ujerumani inajiwekea rekodi ya aina yake - haijawahi kukosa hatua ya robo fainali tangu karne hii ianze,
Bao la Ujerumani lilifungwa dakika ya 13 na beki wa kati Mats Hummels kufuatia krosi ya mpira wa adhabu uliopigwa na kiungo Toni Kroos.
Mats Hummels akiruka juu kufunga bao
Hummels anafanikiwa kuandika bao dakika ya 13
Kipa Lloris anaruka bila mafanikio ...mpira unajaa wavuni
Hummels anashangilia bao lake
Timu nzima ilikwena kumpongeza Hummels
Ufarasansa walihangaika kutafuta bao la kusawazisha lakini kipa Manuel Neuer alikuwa kikwazo kwa kuondoka michomo mingi ya washambuliaji wa vijana wa Didier Deschamps.
Miongoni mwa harakati zilizozimwa na Manuel Neuer ni pale alipookoa shuti la karibu la Karim Benzema dakika ya 90 na kuwa kona isiyozaa.
Ujerumani ilishindwa kutandaza lile soka lake la kuvutia lakini ilikuwa imara katika kumiliki mpira na kutengeneza mashambulizi ya kushtukiza.
Ujerumani sasa itaumana na mshindi kati ya Brazil na Colombia kwenye hatua ya nusu fainali Julai 8.