Baada ya kubainika noti ya shilingi 500 kuwa na mzunguko mkubwa wa matumizi, na kuchakaa kwa haraka huku kiwango chake kudumu kwenye mzunguko kwa miezi sita, Benki kuu ya Tanzania (BOT), inatarajia kubadili noti hiyo na kuwa sarafu.
Sarafu hiyo ya 500 inatarajia kutambulishwa na kuanza kutumika hivi karibuni ikienda sambamba na kipindi cha mwaka huu wa fedha.
Mabadiliko hayo yanatarajiwa kufanyika huku sarafu hiyo ikitarajiwa kudumu kwenye mzunguko kwa zaidi ya miaka 20 na kubaki na ubora
wake ule ule.
wake ule ule.
Afisa mkuu wa benki kitengo cha idara kurugenzi za kibenki, Patrick Fata, amenukuliwa akisema kuwa "Tunafanya hivi kwasababu noti ya 500 inachakaa haraka kulinganisha na mzunguko wake na kuwafikia watu wengi na kuchakaa haraka, utengenezaji wake ni ule ule ila inachaa kutokana na mzunguko inaweza kushikwa na watu milioni moja kwa siku kuliko noti ya elfu 10."
"Inaanza kutumika mwaka huu wa fedha inategemea kutoka Julai mwaka huu."