Akizungumzia sakata la kuibuka kwa watu wanaojitangaza kuwania urais, Askofu mstaafu ndugu Valentine Mokiwa amesema kuwa nchi ya Tanzania bado ni changa sana hivyo haipaswi kuongozwa na wanyoa 'unga' maarufu kama 'vipara'.
"Nchi yetu bado ni changa sana hivyo sii busara kuongozwa na wanyoa 'unga'.Tunahitaji damu iliyokomaa kutuongoza". Alisema Mokiwa huku akionekana dhahiri kumlenga mmoja wa watu ambaye ametangaza nia ya kuwania urais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania hivi karibuni kupitia kituo kimoja maarufu duniani cha runinga ya idhaa ya Kiswahili.