SEHEMU ambayo inasemekana bomu lilitua mara baada ya kutupwa.
Mkurugenzi wa tiba ambaye pia ni kaimu mgamga mkuu wa hospitali ya Seliani Dr. Paulo akiongea na waandishi wa habari |
Na Woinde Shizza,Arusha.
Mlipuko unaosadikiwa ni bomu umelipuka usiku wa kuamkia leo jijini Arusha katika mgahawa wa Traditional Indian Cusine uliopo pembezoni mwa hotel ya Gymkana jijini hapa na kujeruhi watu nane.
Akithibitisha kupokea wagonjwa walioathiriwa na bomu hilo, Mkurugenzi wa tiba ambaye pia ni kaimu mganga mkuu wa hospitali ya Seliani Dr. Paulo Kisanga alisema kuwa tukio hilo lilitokea majira ya saa 4:30 usiku katika eneo kwani walianza kupokea wagonjwa hao kuanzia majira ya saa tano kasoro na saatano .
Alisema kuwa walipokea wagonjwa nane ambao waliumia sana katika maeneo ya miguu ambapo alibainisha kuwa katika wagonjwa hao na ne kuna mmoja ambaye aliletwa akiwa na hali mbaya sana kitu ambacho kiliwalazimu kumfanyia upasuaji usiku huo huo.
"kati yawagonjwa hao nane,mmoja alikutwa akiwa mahututi ,kwani mguu wake ulikuwa umeathiriwa sana na bomu hilo ,ivyo ikatulazimu kumkata mguu mmoja wa kushoto ,mgonjwa huyo ambaye tumemkata mguu anaitwa Deepak Gupta (25) mwanaume,na sasa ivi anaendelea vyema kidogo na yupo katika chumba cha ICU ndani ya hospitali hii yetu ya Seliani"alisema Kisanga
Alisema kuwa katika majeruhi au nane aliowapokea wanawake wako watatu huku wanaume wakiwa watano na kubainisha kuwa wote wameshafanyiwa upasuaji na wapo wodini kwa ajili ya uangalizi wa madaktari
Aidha aliwataja majeruhi hao kwa majina kuwa ni pamoja na Vinod Suvesh(37), Ritwik Khandelval (13),Raj Rajin(30),Prateck Saver,manci Gupta(14) ,Manisha Gupta (36),Mahush Gupta(42) pamoja na Deepak Gupta (25) wote wakiwa na asili ya kiasia.
Kisanga alisema kuwa kwa mujibu wa wagonjwa hao walio waliofika hapo hospitali walidai kuwa bomu hilo lilirushwa kwa kupitia dirishani.