Katika michuano ya kombe la dunia kumeibuka wachezaji wengi ambao wameonyesha uwezo mkubwa kiasi cha kuteka hisia za watu wengi, mmoja wapo ni golikipa wa Mexico Guillermo Ochoa.Golikipa huyu alionyesha uwezo mkubwa katika mechi alizoichezea Mexico kwenye michuano ya kombe la dunia inayoendelea nchini Brazil, kabla ya timu yake kutolewa na Uholanzi katika hatua 16 bora – lakini pamoja na kuondolewa kwa timu yake bado uwezo wake umeacha gumzo kubwa sana kwenye michuano hii.
Uwezo aliouonyesha Ochoa ulipelekea kuzuka kwa taarifa kwamba golikipa huyo wa Mexico aliumbwa akiwa na vidole sita vya mkononi. Zikatolewa mpaka picha kupitia vyombo vya habari mbalimbali ambavyo vilimuonyesha Ochoa akiwa na vidole sita.
Lakini ukweli ni kwamba kipa huyo ambaye kwa sasa anawindwa na vilabu vingi hana vidole sita. Picha zilizoonyeshwa na kusambazwa kwenye vyombo vya habari ni za kutengeneza.