Thursday, July 03, 2014

NSSF YAPANUA WIGO WA HUDUMA ZAKE KWA KUANZISHA MPANGO MAALUMU KWA WAKULIMA NA WACHIMBA MADINI WADOGO



NSSF YAPANUA WIGO WA HUDUMA ZAKE KWA KUANZISHA MPANGO MAALUMU KWA WAKULIMA NA WACHIMBA MADINI WADOGO
Kaimu Mkurugenzi Mkuu, Crescesius Magori (kulia) wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF akipata maelezo kutoka kwa Meneja Kiongozi, Uhusiano na  Huduma kwa Wateja, Eunice Chiume (katikati) wa Shirika hilo alipotembelea banda hilo katika Maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba). Wa pili kulia ni Mkurugenzi wa Mawasiliano na  Teknohama, Idi Khalfani, Kushoto ni Afisa Uhusiano Mwandamizi, Teopista Muheta.
Kwa sasa Wakulima na wachimba madini Wadogo wanaweza kujichangia na kufaidika na mafao mbalimbali yatolewayo na NSSF.Kwa maelezo zaidi tembelea Banda la NSSF lililopo katika maonyesho ya sabasaba, kwa wanachama na wasio wanachama wa NSSF wote wanakaribishwa.
Afisa wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii–NSSF Mwadawa Asibawi  akitoa maelekezo kuhusu mikopo kupitia SACCOS inayotolewa na Shirika hilo kwa wanachama wake, Abdallah Majura. Katika mpango huo, wanachama wanaweza kufaidika na mikopo hiyo ikiwa ni mpango wa serikali wa kuwawezesha wanachama wa mfuko huo kupambana na umasikini.
Maafisa wa Shirika la Hifadhi ya jamii NSSF akisikiliza kwa umakini swali alilokuwa akiulizwa na mwanachama kuhusu mradi wa DEGE ECO VILLAGE katika maonyesho ya Sabasaba.Katika mradi huo wanachama wanaweza kununua nyumba za kisasa na nafuu. Kushoto ni Julius Nyamuhokya, Jumanne Mbepo(katikati) Na Aly Chwaya ( kulia)
 Ofisa Uhusiano wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Christina Msengi akitoa maelezo kuhusu  Mafao ya uzazi yatolewayo na Shirika hilo. Mafao haya hutolewa kwa wanachama wanawakee wanaotegemea  kujifungua(wajawazito) au wameshajifungua.
Afisa Uhusiano wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Devotha Ikandilo (kulia), akizungumza na mwanachama kuhusu huduma mbalimbali zitolewazo na shirika hilo. Kwa sasa wakulima na wachimba madini wadogo wadogo wanaweza kujiunga na mfuko huu na kuweza kufaidika na mafao mbalimbali yatolewayo na shirika hilo yakiwemo mafao ya matibabu, mafao ya kuumia kazini na mafao ya uzeeni.
  Afisa uhusiano wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Said Mohamed akitoa maelezo kuhusu mafao ya matibabu yatolewayo na Shirika hilo. Kwa sasa wafanyakazi na wale walio katika sekta isiyo rasmi wanaweza kuchangia mfuko huo na kufaidika na mafao ya matibabu yatolewayo na Shirika hilo.