Naibu Waziri wa Fedha wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mwigulu Nchemba ( Mb) akizungumza wakati wa majadiliano kuhusu masuala ya Ushirikiano wa Kimaendeleo uliofanyika kwa siku mbili hapa Umoja wa Mataifa. Mhe. Naibu Waziri alikuwa mmoja wa wanajopo wanne walioendesha majadiliano hayo. Katika mchango wake, Naibu Waziri pamoja na mambo mengine amesisitiza kuwa Ushirikiano wa Kimaendeleo bado una mchango mkubwa katika ufanikishaji wa suala zima la maendeleo endelevu lakini akataka iwemo mifumo ya ufuatiliaji ambayo itakuwa jumuishi.
Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi ambaye alifuatana na Mhe. Naibu Waziri katika mkutano huo. Aliyeketi nyuma ya Balozi Manongi, ni Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiwano wa Kimataifa, Balozi Celestin Mush na pembeni ya Balozi ni msaidizi wa Naibu Waziri.
Ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambao kwa takribani wiki mbili umekuwa ukihudhuria na kushiriki mikutano na mijadala mbalimbali inayohusu mwelekeo wa ukamilishwaji wa malengo ya maendeleo ya milenia ( MDGs), mchakato wa maandalizi ya ajenda na malengo mapya ya maendeleo endelevu baada ya 2015 na Ushirikiano wa Kimaendeleo. Mikutano hiyo imeandaliwa na Balaza la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya Uchumi na Maendeleo ya Jamii ( ECOSOC)
Sehemu ya washiriki waliokuwa wakifuatilia majadiliano hayo na ambapo baada ya wanajapo kutoka mchango wao walipata fursa ya kuuliza maswali au kuchangia maoni yao. Mkutano huu wa siku mbili kuhusu Ushirikiano wa Kimaendelea umefanyika nchi na mwamvuli wa ECOSOC
wajumbe walioshiriki majadiliano kuhusu Ushirikiano wa Kimaendeleo wakifuatilia majadiliano hayo.