Sunday, July 06, 2014

MWENYEKITI WA TACIN ANIC KASHASHA ATEMBELEA BANDA LA TPDC SABASABA



MWENYEKITI WA TACIN ANIC KASHASHA ATEMBELEA BANDA LA TPDC SABASABA
Mwenyekiti Mtendaji we shirika lisilo la kiserikali la TACIN, Bw. Anic Kashasha,(katikati) akiwa pamoja na uongozi wa juu wa Shirika la Maemdeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) akiwemo Mkurugenzi Mtendaji Bw. Yona Kilaghane (wa pili kulia) na Bibi Joyce Kisamo, Mkurugenzi wa Masoko na Uwekezaji, alipotembelea banda la shirika hilo kwenye viwanja vya Saba Saba jijini Dar ea Salaam, mapema leo. 
TACIN ni washirika wa TPDC kwenye maandalizi ya Mtwara Festival ambayo ni mkakati wa mawasiliano wa kuhamasisha jamii ya Wananchi wa mikoa ya Mtwara na Lindi, kizitambua fursa shirikishi zinazotokana na uongezekaji mkubwa wa uwekezaji katika mikoa hiyo kutokana na uchumi mkubwa wa gesi asilia ili wajiandae na kuzichangamkia.  Mtwara Festival 2014 itafanyika katika viwanja vya Nangwanda Sijaona, tarehe 16 na 17 Agosti, 2014 mjini Mtwara. 
Mtwara Festival itakuwa ni mchanganyiko wa mawasiliano, michezo mbalimbali, maonyesho ya utalii, huduma na bidhaa. Washiriki wanakaribishwa kutoka sekta zote. Hayo yote yatasindikizwa na burudani kutoka kwa wasanii na vikundi mbalimbali.