Friday, July 18, 2014

Miili zaidi ya 100 yaokotwa baada ya ndege ya Malaysia 'Kutunguliwa' Ukraine




Miili zaidi ya 100 yaokotwa baada ya ndege ya Malaysia 'Kutunguliwa' Ukraine

Mabaki ya miili zaidi ya 100 yameokotwa jirani na eneo 
ilipoangukandege ya Malaysian Airlines kule Grabovo jirani na mpaka wa 
Ukraine na Urusi .Reutersiliripoti mapema Alhamisi kuwa ndege hiyo 
yenye namba MH17 ilianguka jimboni Donetsk ikiwa njiani kuelekea Kuala 
Lumpur ikitokea mjini Amsterdam, Uholanzi.Kuna taarifa zisizo rasmi 
kuwa ndege hiyo 'imetunguliwa' na aidha majeshi ya Ukraine, ama waasi 
wanaoiunga mkono Urusi, vyanzo mbalimbali vya habari 
vimeripoti.Waokoaji wamesema miili imeokotwa katika eneo la umbali 
unaozidi kilometa15 toka ndege ilipoanguka."Hatuwezi kuthibitisha kama 
ndege hiyo imetunguliwa ama la,"alisema Rais wa Ukraine Petro 
Poroshenko."Hata hivyo, tunasisitiza kuwa Ukraine haijarusha makombora 
yoyote angani leo,"aliongeza.Katika taarifa iliyotolewa mapema leo, 
Malaysian Airlines ilidai ilipoteza mawasiliano na ndege hiyo mnamo 
saa 8 na dakika 15 GMT.Tovuti yaThe Guardianinaripoti kuwa vyanzo toka 
ndani ya Wizara ya Mamboya Ndani ya Ukraine vinadai ndege 
hiyoilitunguliwa na kombora toka mfumo wa kurusha roketi hewani 
unaojulikana kama BUK.Teknolojia ya BUK ilikuwa maarufu sana Urusi 
miaka ya 1970, na ilirithiwa na bado yaendelea kutumika na zile 
zilizokuwa Jamhuri za Kisovieti, ikiwamo Ukraine.Wachambuzi sasa 
wanahoji walorushakombora hilo wamelipataje, huku baadhi wakidai hiyo 
ni uthibitisho tosha kuwa waasi wanaoiunga mkono Urusi wako nyuma ya 
'shambulizi' hilo.Kati ya watu 295 walokuwa ndani ya ndege hiyo aina 
ya Boeing 777, 280 walikuwa abiria na walobaki ni wahudumu na 
marubani.Picha zilizotupwa katika mitandao ya kijamii na tovuti 
mbalimbali zinaonyesha masalia ya ndege hiyo yenye rangi za bluu na 
nyekundu yakifuka moshi.Picha hizo zimeamsha hisia kali, zikiukumbusha 
umma kuhusu ajali nyingine inayohusisha ndege ya Malaysia namba MH370 
ilopotea toka Machi, huku ikiwa haijaonekana.Mataifa mbalimbali 
yanaendelea na jitihada za kutathmini kama raia wake walikuwamo ndani 
ya ndege 'ilotunguliwa,' huku baadhi ya mashirika ya ndege, ikiwemo 
Emirates, Lufthansa, British Airways na Aeroflot, yakisitisha safari 
zote kwenya anga la Ukraine.Chanzo: Mwananchi