

.
Sehemu ya ujumbe wa Mawaziri wa Fedha,Biashara na Uwezeshaji kutoka Nchi mbalimbali za SADC wakiendelea na Majadiliano kuhusu Uwezeshaji wa Kifedha ndani ya Jumuia hiyo.


Pamoja yakiendelea kwa Wajumbe Watatu Kutoka Tanzania kwenye Kikao cha SADC hapa Gaberone.







Gaberone-Botswana.
SADC imefanya mkutano wake uliojumuisha sekta tatu tofauti,Fedha,Biashara na Uwezeshaji nchini Botswana Mji wa Gaberone,Mkutano ulioanza Tar.11/07/2014 na kumalizika hii leo Tar.18/07/2014.
Tanzania katika mkutano huo imewakilishwa na Mawaziri kutoka Hazina(Mh:Mwigulu Nchemba),Waziri wa Uwekezaji na Uwezeshaji Ofisi ya Waziri Mkuu Mh:Marry Nagu na Waziri wa viwanda na Biashara Mh:Abdallah Kigoda.Mkutano huu wa SADC Umejikita kwenye majadiliano ya kufikia makubaliano ya kuanziasha kwa biashara huria na kuondoa vikwanzo mf.Ushuruwa forodha n.k.(Boosting Inter-African Trade-BIAT).
Pia kuanzishwa kwa mfuko wa kifedha utakaowezesha jumuia ya SADC kuendesha miradi yake ya maendeleo kwa ufanisi katika Nchi wanachama wake.Agenda ya kuanzishwa kwa mfuko wa kifedha ilianza kujadiliwa kwenye kikao cha SADC Kilichofanyika Maputo-Mozambique mwaka 2012 na 2013.
Picha/Maelezo na Festo Sanga
Gaberone-Botswana.